Tume ya Ulaya imeitaka Hispania kueleza ambavyo muuguzi huyo aliambukizwa Ebola na kuzua hofu ulaya
Tume
ya Ulaya imeitaka Uhispania kueleza ambavyo muuguzi aliambukizwa Ebola
mjini Madrid na kumfanya kuwa mtu wa kwanza kuambukizwa ugonjwa huo
nchini humo kutoka Afrika Magharibi.
Muuguzi huyo ambaye amewekwa
karantini alikuwa sehemu ya kukindi cha matabibu waliowatibu wamishonari
wawili waliofariki kutokana na ugonjwa huo nchini humo.
Maafisa wa Afya nchini hispania wanasema kuwa muuguzi huyo anapokea matibabu.
Maafisa
wakuu wanasema kuwa watu wnegine watatu wanachunguzwa hospitalini baada
ya kushukiwa kuwa na dalili za Ebola. Watatu hao ni pamoja na mumewe
muuguzi huyo , mfanyakazi mwingine wa afya na msafiri mmoja kutoka
Afrika Magharibi.
Afisa mmoja wa afya nchini Hispania anasema kuwa muuguzi huyo angetengwa awali baada ya kugundulika kuwa na virusi hivyo.
Takriban watu 3,400 wamefariki kutokana na Ebola wengi wao wakiwa Afrika Magharibi.
Muuguzi
huyo mwenye umri wa miaka 40,ambaye hajatajwa alikuwa anafanya kazi
katika hospitali ya Carlos 111 mjini Madrid na alihusika katika juhudi
za kuwatibu makasisi Maneul Garcia na Miguel Pajares waliofariki
kutokana na Ebola.
Wote waliambukizwa Ebola wakiwa nchini Liberia katika shughuli za kimishionari.
Muuguzi
huyo aliingia katika chumba alimokuwa mmoja wa wamishionari hao
kumhuduumia na kusaficha chumba hicho baada ya kifo cha mmoja wao. Hata
hivyo nyakati zote alipokuwa anafnya kazi yake alikuwa amevalia magwanda
ya kujikinga kutokana na maambukizi
Maafisa wa afya wanasema
hawajui chanzo cha maambukizi kwa muuguzi huyo maana alikuwa amevalia
magwanda na hapoakuwa na taarifa za ajali yoyote iliyomuweka muuguzi
huyo katika hatari ya kuambukizwa.

إرسال تعليق