KIUNGO
mchezeshaji wa Chelsea Cesc Fabregas amemmiminia sifa kibao
mshambuliaji Eden Hazard na kusema huyo ndiyo Lionel Messi wa Chelsea.
Hazard
aling’ara na Chelsea msimu uliopita na akawa kwenye kiwango cha hali ya
juu kwenye mechi dhidi ya Arsenal weekend iliyopita Stamford Bridge.
Alikuwa
ni Mbelgiji huyo ndiye aliyebadili mchezo na kusababisha penalti ambayo
aliipiga mwenyewe na kuzaa bao la kwanza la Chelsea.
Akizungumza
na Radio Cope kuelekea mechi ya Hispania dhidi Slovakia kwenye kufuzu
Euro 2016, Fabregas ndiyo mtu anayeleta tofauti Chelsea.
“Hazard ana uwezo mkubwa wa kuwavuruga wapinzani,” alieleza Fabregas ambaye alijiunga na kikosi cha Mourinho msimu huu kwa pauni milioni 27.
“Yeye ni kiunganishi kikubwa kwetu kati ya safu ya ushambuliaji na kiungo, ni Messi wetu kwa sababu analeta utofauti.”
إرسال تعليق