Usajili
wa kumleta Neymar Dos Santos katika klabu ya FC Barcelona uligubikwa na
utata mkubwa na hatimaye ulimgharimu Sandro Rosel kazi yake ya urais
katika klabu hiyo ya Catalunya.
Mwanzoni ilitangazwa kwamba ada ya €57m ililipwa kwa usajili wa
Neymar, lakini katika matukio ya hivi karibuni yanaonyesha dili hilo la
uhamisho limeiigharimu klabu zaidi ya €100k, Rosell bado chini ya
uchunguzi kutokana na tuhuma hizi.
Gazeti la Cadenas Ser limetoa taarifa kwamba Rosell amemwambia Jaji
wa kesi yake wiki hii kwamba klabu yake ililipa kiasi cha €300,000
kuwasafirisha marafiki wa Neymar kutoka Brazil mpaka Barcelona kwa
kutumia ndege binafsi katika utambulisho wa Neymar.
Kundi la marafiki wa Neymar maarufu kama ‘The ‘Toiss’ wamekuwa na
Neymar tangu utotoni katika mitaa ya jiji la Sao Paulo, na wamekuwa
wakimtembelea Neymar jijini Barcelona, lakini sasa ni mchezaji mwenyewe
anayewalipia washkaji zake.
Post a Comment