Mwili wa Jambazi hilo ukiwa umelazwa ndani ya gari la polisi mara baada ya kuwawa tayari kwa ajili ya kupelekwa mochwari
picha
ya juu na chini wananchi wa jiji la Arusha waliojitokeza kuuangalia
mwili wa jambazi huyo atari aliowawa na polisi usiku wa kuamkia leo
wananchi wakiendelea kushuhudia mwili wa jambazi hilo nje ya jengo la makao makuu ya polisi mkoani Arusha
baadhi ya vitu vilivyokutwa kwa jambazi hilo zikiwemo silaha mbalimbali
kamanda wa polisi akionyesha moja ya kifaa cha kufanyia tageti kabla ya kupiga kijulikanacho kwa jina laGlock Fab Defence moja ambacho jambazi hilo lilikuwa likitumia
Jambazi
mmoja aliefahamika kwa jina la Ramathan Abudallah alimaarufu kwa jina
la Ramadhani Ndonga (37) mkazi wa Moivo ameuwawa baada ya kupigwa
risasi katika majibizano na askari wa jeshi la polisi.
Akizungumzia
tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas Alisema kuwa
tukio hilo limetokea October 10 mwaka huu majira ya saa nane na dakika
nne usiku katika kijiji cha Moivo kilichopo ndani ya kitongoji
cha Enaboishu wilayani Arumeru.
Alisema
kuwa marehemu Ramadhan Abdallh aliuwa anatafutwa kwa muda mrefu na
jeshi la polisi kwa kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu ambayo
yameshawahi kutokea ndani ya mkoa huu pamoja na katika maeneo mbalimbali ya nchi hiii.
Alibainisha
kuwa kuuwawa kwa jambazi hili kumetokana na juhudi na kutumia mbinu za
kisasa za kiyupelelezi na kufika nyumbani kwa mtuhumiwa (marehemu)
ambapo askari polisi walimwamuru ajisalimishe lakini alikaidi amri na
kuanza kuwarushia risasi hali ambayo ilisababisha askari kujibu
mashambulizi na kumsababishia umauti kumfika.
“Mara
baada yakupiga jambazi huyo polisi walianza kumpekuwa mwili wa
marehemu na alipatiana akiwa ba bastola aina ya Glock 19 yenye namba
RLU976 iliotengenezwa nchini Austria ikiwa na magazine yenye risasi (14)
ambapo alikuwa ameishika mkononi pamoja na maganda matano yarisasi na
mbali na hapo polisi pia walifanya upekuzi katika chumba cha jambazi
hilo na kukuta magazine ingine moja yenye risasi (15) na magazine
zingine mbili zenye uwezo wa kubeba risasi thelathini kila moja ,Radio
call moja yeye nembo ya ITSS/UNICTR pamoja na pikipiki aina ya toyo
power king rangi nyekundu yenye namba za usajili T507 BSU pamoja na
kofia ngumu”alisema Sabas
Aidha
alibainisha kuwa pia katika upekuzi huo wa ndani ya nyumba ya jambazi
hilo pia walifanikiwa kupata pingu moja ,plate namba ingine ya pikipiki
yenye namba za usajili T 805 CVD ambapo alibainisha kuwa jambazi hili
lilikuwa likibadilisha plate namba ya pikipiki kila mara pamoja na
chomba maalumu cha kuwekea magazine pamoja na kufanyia tageti kabla
yakupiga risasi (Glock Fab Defence moja),kifaa cha kusafishia bastola
pamoja na koti kubwa jeusi.
Kamanda
Sabas alitaja baadhi ya matukio ambayo jambazi hili lilishayafanya
kuwa ni pamoja na tukio lililotekea Augast 6 majira ya saa tatu na
nusu usiku maeneo ya kwa iddi ambapo mtuhumiwa akiwa na mwenzake ambaye
ajakamatwa walimpiga risasi ya shingo mwanamke aliyefahamika kwa jina
la Shamimu Rashid aliyekuwa mkazi wa sakina wakati akijiandaa kuingina
nyumbani kwake ,hu ku tukio lingine likiwa limetokea Augast 21 saa
19:00 maeneo yaoasiti ambapo jambazi huyo akiwa na mwenzake kwenye
pikipiki walimjeruhi kwa kumpiga risasi yam domo na kutokea kichwani
mototo aitwaye Christen NIckson mwenye umri wa miaka mitatu na nusu na
kisha kufanikiwa kumpora TSH 2000 na baadae majeruhi kufariki dunia
akiwa anapatiwa matibabu.
Kamanda
sabas alitumia nafasi hiyo kuwapongeza askari wake kwa kufanya kazi
nzuri pamoja na kuwahaidi wananchi kuendelea kufanya uchunguzi na
kuwabaini wahalifu wote na kuwachukulia sheria kali.
“arusha
sio sehemu ya kuifadhi wahalifu ivyo tutajitaidi kwa hali na mali
kuhakikisha tunawamaliza majambazi wote pamoja na wahalifu wote na
napenda kuwaaambia wahalifu waache mapema maana sasa ivi tumejipanga
vilivyo ,pia napenda kuchukuwa nafasi hii kuwaomba wananchi pia
waendelee kuwafichua wahalifu popote pale ili tuwaangamize
kabisa”alisema Sabas
Mmoja
wa wananchi ambaye alijitokeza kushuhudia maiti ya jambazi hilo
Aliyejitambulisha kwa jina la Alaija Saro akiongea na libeneke blog hili
alilipongeza jeshi la polisi kwa kuweza kumuangamiza jambazi hilo
kwani limekuwa likiwatia mashaka watu wengi na kuwanyima raha kwa jinsi
walivyokuwa wanauwa watu.
habari picha kwa hisani ya woindeshizza blog
إرسال تعليق