MSHAMBULIAJI
wa Chelsea Diego Costa amefanikwa kufunga bao lake la kwanza kwa timu
ya Taifa pale Hispania ilipoifumua Luxembourg 4-0 katika mchezo wa
upande mmoja wa kufuzu Euro 2016.
Kumbukumbu
zinaonyesha kuwa hakuna namba 9 mwingine wa Hispania aliyechukua muda
mrefu kufunga bao la kwanza kwa timu ya taifa kama ilivyomchukua Costa.
Imemchukua Costa dakika 515 kuifungia Hispania ambayo si nchi yake ya kuzaliwa.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alifunga dakika ya 69 likiwa ni bao la tatu baada ya David
Silva na Francisco Alcacer kufunga mabao mawili ya kipindi cha kwanza
huku Juan Bernat akihitimisha kwa goli la dakika ya 88.
Kipa wa Manchester United David De Gea akasimama langoni ikiwa ni mwanzo wa kuanza kurithi mikoba ya Iker Casillas ambaye amekuwa kwenye kiwango kibovu kupitiliza.
Luxembourg:
Joubert, Mutsch, Chanot, Martins Pereira (Turpel, 60), Philipps,
Janisch, Jans, Gerson, Holter, Da Mota Alves (Payal, 75), Bensi
Spain:
De Gea, Pique, Bartra, Jordi Alba, Carvajal, Busquets, Iniesta (Bernat,
72), Koke, Silva (Pedro, 71), Alcacer, Costa (Rodrigo, 83)
Post a Comment