Watu watatu wamefariki na wengine sita wakiwa
katika hali mbaya Hospitali ya Muhimbili kufuatia tukio la moto
uliolipuka kwenye gari la kubeba mafuta jana maeneo ya Mbagala jijini
Dar es Salaam.
Alizumgumza na mwandishi, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu
Kamishna Mohammed Mpinga, alisema ajali hiyo haikuleta athari yoyote
baada ya gari lile kupata ajali ila athari ilijitokeza baada ya watu
kuvamia na kuanza kuiba mafuta na baadaye kujaribu kuiba betri ndipo
cheche za moto zilipolipuka na kusababisha kuwaka kwa gari hilo.
Wakati huohuo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mecky Sadick,
amewataka wananchi kutokuwa na tabia ya kuvamia ama kuiba vitu pindi
ajali zitokeapo.
Sadick alisema hayo alipotembelea hospitali ya Muhimbili na Temeke walipolazwa majeruhi hao.
picha na gpl
Post a Comment