Sehemu
ya Mabaki Lori la mafuta lililoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo
mara baada ya kupiga mweleka likiwa katika hatakati ya kulikwepa gari
lingine lililokuwa likitokea Kongowe ambalo liliingia ghafla barabarani
bila ya tahadhari,hali iliyolipelekea Lori hilo kukosa mwelekeo na
kupiga mwereka.
Lori hilo
pamoja na kupiga kwake mweleka halikuwa na madhara yeyote wala dalili
ya kusema litawaka moto.Baada ya muda likaja kundi la vijana likiwa na
madumu na mifuko ya plastiki na kuanza kuchukua mafuta yaliyokuwemo
kwenye lori hilo hali iliyopelekea kutokea mlipuko mkubwa ulioliteketeza
lori hilo.
haijafahamika
mpaka sasa kama kuna mtu yeyote aliepoteza maisha katika moto huo,ila
hasara kubwa imeonekana kutokea kwa nyumba tatu zilikuwepo jirani na
eneo la tukio zimeteketea kwa moto,ambazo moja ni ya makazi ya watu,duka
la juma la Mchele pamoja nyumba ya kulala wageni.
Sehemu ya Wakazi wa Maeneo hayo wakiangalia kilichotokea huku wakiwa hawaamini wanachokiona.
Sehemu ya Nyumba zilizoteketea kwa moto.
Sehemu ya Nyumba zilizoteketea kwa moto.
Post a Comment