Wakiwa hawajapoteza mchezo wowote katika ligi kuu ya Hispania mpaka
sasa huku wakiongoza ligi hiyo, FC Barcelona leo walijitupa uwanjani
kupambana na Rayo Vallecano kwenye dimba la Estadio del Rayo Vallecano.
Huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mechi yao Champions League
dhidi ya Paris Saint Germain, FC Barcelona waliingia uwanjani wakitaka
kuendeleza rekodi yao kushinda mechi zao zote za La Liga.
Matokeo ya mchezo huo ulioisha hivi punde ni ushindi wa 6 kwa vijana
wa Luis Enrique katika mechi 7 za ligi walizocheza msimu huu.
Magoli ya Lionel Messi na Neymar yaliisadia Barca kufikisha jumla ya
pointi 19 katika La Liga na kuendelea kushikilia kilele cha msimamo wa
ligi hiyo.
Takwimu za Mechi:


Post a Comment