
Kila mmoja 
amekua na hofu akisikia au kukutana na mtu alietoka kwenye nchi 
zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola barani Afrika na ndio maana ubaguzi 
umeripotiwa katika nchi mbalimbali za Amerika, Ulaya na hata Afrika 
ikijulikana unatokea Afrika.
Ripoti mpya inasema Mwanamke mmoja wa Kenya amefia kwenye uwanja wa 
ndege Jomo Kenyatta Nairobi kwa tetesi kwamba alikua anaumwa Ebola au 
Marbug ambapo familia yake imeilaumu Serikali kwa kifo cha ndugu yao kwa
 kutelekezwa na wauguzi kwenye Clinic ya uwanja wa ndege waliokua na 
hofu ya kuambukizwa ugonjwa wa Ebola.
NTV Kenya wameripoti kwamba Marehemu ambae alikua mfanyabiashara 
aliondoka nchini Kenya na kuelekea Juba Sudan ambapo alipitia Uganda 
wakati mlipuko wa Marburg ulipotokea na alipowasili Juba alikua anavuja 
damu kwenye sehemu ya uzazi jambo lililofanya dada yake amrudishe 
Nairobi kwa ajili ya matibabu.

Baada ya ndege kutua tu Familia yake inasema hakuhudumiwa ipasavyo 
ambapo kwa muda wa dakika 120 Mama yake mzazi na rafiki yake walibaki 
kutazama tu hali yake ikiendelea kudorora na alikua akilalamika anaumwa 
kichwa na amemiss mtoto wake wa kiume. 
Mama Wanjiku pamoja na rafiki yake pamoja na Marehemu waliwekwa 
kwenye chumba kimoja kwa zaidi ya saa tano kabla ya kuruhusiwa kuondoka 
ambapo Wanjiku alifariki dunia akiwa kwenye kiti cha magurudumu. 
Mama mzazi na rafiki yake waliruhusiwa kuondoka kabla ya matokeo ya 
uchunguzi wa matibabu kutolewa, kama Marehemu alikua akiugua Ebola au 
Marburg basi kuachiliwa kwao kungepelekea kusambaa kwa ugonjwa huo kwa 
haraka…
إرسال تعليق