Hot:- Ajali mbaya Mbezi Mwisho (Dar): Basi la Najimunisa lagongana na Land Cruiser

Picha si Halisi
Usiku huu eneo la Darajani hapa Mbezi Mwisho,Basi la Kampuni ya Najimunisa limegongana uso kwa uso la gari ndogo aina ya Land Cruiser hard Top.
Ajali imetokea majira ya Saa tano usiku,Basi la Najimunisa likiwa "limetanua" njia likitokea Mwanza likakutana uso kwa uso na Land cruiser iliyokuwa katika "sight" yake.
Basi limetumbukia korongoni juu chini,Majeruhi ni wengi na Polisi wamelazimika kutumia risasi za moto kuwatawanya "vibaka" waliotaka kutumia mwanya huo kuwapora majeruhi wa ajali.
Uokozi unaendelea na majeruhi wengi wanapelekwa hospital,mpaka sasa hakuna kifo kilichoripotiwa,Magari ya "BreakDown" wanajitahidi kulitoa basi chini ya korongo

- JF

Post a Comment

Previous Post Next Post