
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limesema
kuwa, kundi la kigaidi la Boko Haram linawalazimisha wasichana
waliowateka nyara kwenda vitani ili kusaidia mashambulio yao.
WRH imesema hayo kutokana na ushahidi uliotolewa na makumi ya wasichana
waliokuwa wametekwa nyara, wanaosema kwamba walipata mateso ya
kisaikolojia na kimwili kutoka kwa wafuasi wa kundi hilo.
Katika ripoti ya shirika hilo la kutetea haki za binadamu, msichama
mmoja mwenye umri wa miaka 19 aliyekuwa akishikiliwa na Boko Haram kwa
mwaka moja amesema kuwa alilazimishwa kushiriki katika mashambulio ya
kundi hilo.
Mwishoni mwa wiki hii vijana wengine 30 walitekwa nyara na kundi la Boko
Haram katika jimbo la Borno huko Nigeria. Vijana hao waliotekwa nyara
ni mchanganyiko wa wavulana na wasichana wenye umri wa kati ya miaka 11
na 13.
Shirika la Human Rights Watch linakadiria kuwa, zaidi ya wanawake na
wasichana 500 wametekwa nyara na kundi hilo tangu lilipoanza
mashambulizi yake mwaka 2009.
Chanzo: kiswahili.irib.ir
Post a Comment