HRW: Boko Haram wanatumia waliowateka vitani

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limesema kuwa, kundi la kigaidi la Boko Haram linawalazimisha wasichana waliowateka nyara kwenda vitani ili kusaidia mashambulio yao.

WRH imesema hayo kutokana na ushahidi uliotolewa na makumi ya wasichana waliokuwa wametekwa nyara, wanaosema kwamba walipata mateso ya kisaikolojia na kimwili kutoka kwa wafuasi wa kundi hilo.

Katika ripoti ya shirika hilo la kutetea haki za binadamu, msichama mmoja mwenye umri wa miaka 19 aliyekuwa akishikiliwa na Boko Haram kwa mwaka moja amesema kuwa alilazimishwa kushiriki katika mashambulio ya kundi hilo.

Mwishoni mwa wiki hii vijana wengine 30 walitekwa nyara na kundi la Boko Haram katika jimbo la Borno huko Nigeria. Vijana hao waliotekwa nyara ni mchanganyiko wa wavulana na wasichana wenye umri wa kati ya miaka 11 na 13.

Shirika la Human Rights Watch linakadiria kuwa, zaidi ya wanawake na wasichana 500 wametekwa nyara na kundi hilo tangu lilipoanza mashambulizi yake mwaka 2009.

Post a Comment

أحدث أقدم