
Kiungo
wa timu ya Azam, Salum Abubakar amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa
mwezi Oktoba wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi
kwenye viwanja mbalimbali nchini.
Abubakar
ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
aliwashinda wachezaji wengine 20, huku wanne kati ya hao wakichuana naye
kwa karibu.
Wachezaji
hao ni Joseph Mahundi wa Coastal Union, Salim Mbonde (Mtibwa Sugar),
Rashid Mandawa (Kagera Sugar) na Najim Magulu wa JKT Ruvu Stars.
Kwa
kuibuka mchezaji bora, Abubakar atazawadiwa kikombe na fedha taslimu
sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za
mkononi ya Vodacom.
Jopo
maalumu la makocha waliopo katika viwanja vyote vinavyotumika kwa mechi
za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ndiyo wanaofanya kazi ya kuchagua mchezaji
bora kwa kila mechi kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, na baadaye
alama zao kujumlishwa ili kumpata mshindi wa mwezi.
Post a Comment