IGP Mangu ataka amani uhubiriwe kwa vitendo

Picha ya pamoja mkuu wa Jeshi la Police Nchini Erenest Mangu na Viongozi wa Mkoa wa Ruvuma aliye simama kushoto             wa kwanza ni Sheikh Yusufu Kambaulaya

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na  jeshi hilo katika kutokomeza uhalifu.

Alisema pasipo kuwapo na ushirikiano dhana ya  polisi jamii haitafanyakazi iliyokusudiwa na jamii itaishi kwa mashaka.

Kauli hiyo ameitoa Songea hivi karibuni wakati wa wakati wa chakula cha jioni ikulu ndogo mjini hapa.

Alisema ushirikiano ulioonyeshwa na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Dini ndiko kumewezesha nchi hii kuendelea kuwa na amani.

Aliwataka viongozi kuhubiri amani na utii wa sheria bila shuruti hivyo kurahisisha kazi ya jeshi hilo kupambana na uhalifu.,

Akishukuru baada ya kukabidhiwa zawadi mbalimbali ikiwamo Kurani tukufu aliyokabidhiwa na Shehe wa Mkoa wa Ruvuma Yusufu Athumani Kambaulaya  alisema:“Ni juu ya kila Mmoja kuendeleza juhudi za kulinda amani na kuwa msitari wa mbele kushirikiana na Serikali kupinga uhalifu na kuweza kuwaumbua wale wanao endeleza uovu.”

Aliwataka viongozi wa dini kuwahubiria waumini wao namna bora ya kuenzi amani ikiwa na pamoja na kuwuambua wahaklifu wa aina zote bila kujali wadhifa wao katika jamii.

Mchana katika ziara yake mkoani Ruvuma mkuu huyo wa Polisi nchini alikagua Jengo la  Dawati la Jinsia na Watoto  Jengo lililo gharimu shilingi milioni 38.

Jingo hilo ambalo limewezeshwa kwa njia ya msaragambo chini ya kamati ya uhamasishaji  iliyoongozwa na Adamu Mzuza Nindi limeweza kusaidia wanawake na watoto kuwa na faragha katika matatizo yanayowakuta.

Post a Comment

أحدث أقدم