Kikosi cha Yanga.
Na Mashaka Baltazar, ShinyangaWAKATI joto la mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Stand United na Yanga likizidi kupanda miongoni mwa mashabiki wa timu hizo, Stand wameingia mafichoni.
Pambano hilo la kihistoria katika soka la Mkoa wa Shinyanga, litapigwa kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini hapa kesho, likitarajiwa kuwa gumu kutokana na kila timu kujiandaa.
Akizungumza na Championi Ijumaa kwa njia ya simu juzi, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Shinyanga (Shirefa), Benester Lugora, alisema ugumu wa mchezo huo umesababisha waweke kambi yao mafichoni.
“Hatukuwahi kufanya hivi lakini mazingira ya mchezo wa Jumamosi na ugumu wake, yamesababisha tufanye hivi kwa kuiweka timu mafichoni, kuhakikisha tunashinda, kama unavyofahamu mpira, tumejiandaa kwa ushindi, hatujawahi kuiweka timu mafichoni, lakini safari hii tumeamua kufanya hivyo na hatuna hofu na hilo,” alisema Lugora.
Yanga ina pointi saba baada ya kucheza mechi nne wakati Stand ina pointi tano, mechi hiyo inatarajiwa kuwa ngumu kwani pande zote zinaonekana kujiandaa vizuri ambapo Yanga jana ilitua mkoani Dodoma na kuweka kambi ya muda kabla ya leo kuelekea Shinyanga.
إرسال تعليق