
afadhali igizo la BMK limekwisha na sasa watu watajielekeza kwenye ufisadi unaolitafuna Taifa, mfano #TegetaEscrow #IPTL David Kafulila Gabriel Mwang'onda

MATOKEO FEKI YANATANGAZWA HAPA.
Wanasema wamepata theluthi mbili upande wa Znz.
Infact ni matokeo ya kupika kwa wazi na hakuna atakayeyashangaa.
Infact ni matokeo ya kupika kwa wazi na hakuna atakayeyashangaa.
Maswali ya Kujiuliza;
1. Idadi alizotaja Samwel Sitta wakati upigaji kura unaanza, siyo idadi inayotajwa Leo. Kwa mfano Sitta alitangaza wajumbe wote kutoka Znz ni 210, Leo Katibu anasema wajumbe wa Znz ni 216.
1. Idadi alizotaja Samwel Sitta wakati upigaji kura unaanza, siyo idadi inayotajwa Leo. Kwa mfano Sitta alitangaza wajumbe wote kutoka Znz ni 210, Leo Katibu anasema wajumbe wa Znz ni 216.
2. Jana Samwel Sitta alisema ati kuna kura MBILI za wajumbe wa UKAWA
zimeongezeka, Hadi Leo hajataja waliopiga kura hizo ni kina nani. Na
Katibu ametangaza wajumbe wasiopiga kura (UKAWA) ni 65, lakini ukweli,
wajumbe wa UKAWA wasiopiga kura ni 67. Kwa hiyo Samweli Sitta amehesabu
na zile kura zake 2 za wajumbe wasiojulikana.
Suala sahihi ni kuwa, upotezaji huu wa Rasilimali na muda. Sasa unafikia mwisho.
JOHN MNYIKA
Dira ni kuwa na katiba bora itakayojenga Tanzania yenye demokrasia ya
kweli, uhuru wa kweli na maendeleo endelevu kwa watu wake wote. Lakini
uharamia katika mchakato wa katiba mpya umelipasua taifa. Mpasuko huu
unaweza kuwa mgogoro hasi wenye madhara kwa wananchi au mgogoro chanya
utakaoleta mabadiliko nchini.
Maharamia wanashangilia kilevi katika Bunge Maalum baada ya kukamilisha
uharamia dhidi ya rasimu ya katiba ya wananchi kwa kupata theluthi mbili
kwa njia za kiharamia. Katiba iliyopendekezwa kiharamia na kudharau
maoni ya wananchi ni katiba haramu iliyokosa maridhiano na muafaka wa
kitaifa.
Katiba haramu, katiba ya maharamia, katiba ya mafisadi, katiba ya CCM
wahafidhiana na mawakala wake inapaswa kupingwa mtaani na mahakamani kwa
mbinu mbalimbali.
Iwe ni kwa mikutano, migomo, maandamano, mashtaka au katika sanduku la
kura. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba mchakato huu wa mabadiliko ya
katiba ni mwanya wa mabadiliko katika taifa letu.
Theluthi mbili ilianza kutafutwa tangu wakati wa kutungwa kwa Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba, tulipinga muundo wa Bunge Maalum na uteuzi wake;
madhara yake yamedhihirika sasa.
Rais Kikwete akaongezea udhaifu huo kwa kutumia madaraka vibaya kuteua
wanaCCM mahafidhina na mawakala wao kwa wingi katika uteuzi wa wajumbe
wa kundi la 201 kuongezea katika hodhi haramu ya wabunge na wawakilishi
wa chama chake.
Sitta akakamilisha uharamia huo kwa marekebisho haramu ya kanuni za
Bunge Maalum ambayo yaliruhusu kura kupigwa nje ya Bunge hilo na mianya
mingine ya wizi wa kura.
Jana Oktoba Mosi Sitta alilalamikia hatua yangu ya kumtaja yeye, Chenge
na wenzake kuwa ni ‘maharamia’ dhidi ya rasimu iliyotokana na maoni ya
wananchi. Kwa kuwaita maharamia Sitta amelieleza Bunge Maalum kuwa ni
“siasa za kichuo chuo” na kwamba “hatuwezi kushika madaraka kwa mbinu za
kitoto”.
Nimkumbushe Sitta na maharamia wenzake kwamba mwaka 1958 Mwalimu Julius
Nyerere alishtakiwa kwa kuwaita ‘mashetani na maharamia’ wakuu wa wilaya
wa Serikali ya mkoloni. Ninapolitazama Bunge Maalum nakumbuka utetezi
wake mahakamani wa kukiri kutamka maneno hayo kwa lengo la kuitaka
serikali ya kikoloni itupie macho malalamiko ya watu.
Sitta na maharamia wenzake kama wameshindwa hata kuelewa waraka wa
viongozi wa dini na kuuita kuwa “hauna utukufu wa Mungu na wa kipuuzi”,
ni wazi wamelewa madaraka wasaidiwe kwa kupumzishwa.
Leo Sitta, Samia Suluhu na maharamia wengine wanasherehekea kama walevi
ushindi wa muda mfupi walioupata kwa njia za kiharamia ikiwemo kwa
kuwashinikiza na kuwarubuni baadhi ya wajumbe kuhalalisha rasimu haramu.
Andrew Chenge aliyetajwa kwenye orodha ya mafisadi (list of shame)
ndiye aliyeongoza kazi hiyo kuanzia katika Kamati ya Uandishi.
Uharamia huu dhidi ya rasimu ya tume ya mabadiliko ya katiba na maoni ya
wananchi unapaswa kuwa kiunganishi kwa umma kutambua kwamba umoja wa
ukweli na uadilifu unapaswa kuvuka mipaka ya vyama, dini, pande mbili za
Muungano na tofauti zingine.
Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) umeonyesha msimamo wake, Mwenyekiti
na Wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wameonyesha msimamo
wao, baadhi ya viongozi wa dini wameonyesha msimamo wao, baadhi ya
wanaharakati wameonyesha msimamo wao, baadhi ya wajumbe ndani ya Bunge
Maalum wameonyesha msimamo wao; wewe je?
Namna pekee ya kuirejesha rasimu ya katiba ya wananchi katika hali
iliyofikia ni kuikataa katiba haramu na kuwakataa wote waliofanya
uharamia kuwezesha rasimu hiyo kupendekezwa na wote watakao itetea
katiba hiyo.
Muasisi wa CCM alikiambia chama hicho mwaka 1995 kwamba “watanzania wanataka mabadiliko wasipoyapata ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM”. CCM imepoteza mwanya wa kuwapa watanzania mabadiliko kutoka ndani ya chama hicho.
Muasisi wa CCM alikiambia chama hicho mwaka 1995 kwamba “watanzania wanataka mabadiliko wasipoyapata ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM”. CCM imepoteza mwanya wa kuwapa watanzania mabadiliko kutoka ndani ya chama hicho.
Uharamia uliofanywa katika Bunge Maalum una baraka za Katibu Mkuu wa CCM
Kinana na Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete. Uharamia huo ulilenga
kuwezesha Maoni ya CCM yaliyopitishwa na vikao vya juu vya CCM kinyume
na maoni ya wananchi. Hatimaye kwa njia za kiharamia wajumbe wanaojiita
walio wengi wa CCM wamepitisha katiba haramu iliyopendekezwa.
Mwalimu Nyerere aliandika katika kitabu cha Uongozi Wetu na Hatma ya
Tanzania kwamba Rais wa wakati huo Mwinyi alikuwa mtu mwema na mpole
lakini “kiongozi dhaifu”. Akamtakia heri na kuomba asaidiwe amalize
kipindi chake salama. Akatabiri kwamba chini ya CCM na uongozi wake
mbele ni giza tororo.
Rais Kikwete alithubutu kwa kukubali mchakato wa mabadiliko ya katiba
kuanza lakini ameshindwa. Na kwa udhaifu alio uonyesha, kwa vyovyote
vile mchakato huu hauwezi kusonga mbele na kukamilika chini yake.
Udhaifu pekee anao weza kuupunguza kwa sasa ni kusimamia marekebisho ya
15 ya Katiba ya mwaka 1977 kuwezesha uchaguzi huru na haki katika
uchaguzi mkuu wa udiwani, ubunge na urais mwaka 2015 na kuendelea kwa
mchakato wa katiba mpya mwaka 2016 kwa kuzingatia maoni ya wananchi.
Tumtakie heri Rais Kikwete amalize kipindi chake salama; matokeo ya kura
ya katiba haramu iliyopendezwa yatafutwa kwa kupingwa mahakamani ama
kwa njia nyingine.
Mahakama kwa kukosa uhuru wa kikatiba isipotimiza wajibu huo wa
kusimamia haki kwa wakati; katiba haramu iliyopendekezwa itafutwa kwa
sheria maalum itayotungwa na Bunge litakaloongoza nchi baada ya uchaguzi
2015.
Ikiwa watawala wa sasa au wa wakati huo watalazimisha katiba haramu
kwenda kupigiwa kura ya maoni, ni wazi itapigiwa kura ya hapana na
wananchi iwe ni mwaka 2015 au 2016.
Mabadiliko yatafutwe kwa kuwakataa watetezi wote wa katiba haramu
kuanzia kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji mwaka
2014. Mabadiliko yatafutwe kwa kutaka Tume itangaze ratiba ya
uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mwaka 2014 ili kila
mwenye umri wa kupiga kura ashiriki kufanya mabadiliko kupitia uchaguzi
2015 na kura ya maoni.
Kwa wajumbe mlioshiriki kuandika katiba haramu, naheshimu na nakubaliana
na maneno ya Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji
(Mstaafu) Joseph Warioba kwamba tutakutana mtaani.
Dhima ni kuwa na katiba mpya itayoleta uongozi bora, sera sahihi,
mikakati makini na Muungano na Muundo wa Utawala thabiti kwa maendeleo
endelevu.
Nyinyi mkiwa na katiba haramu sisi tutakuwa na rasimu ya wananchi; sauti
ya watu, ni sauti ya Mungu hivyo umma utaamua na historia itatoa hukumu
kwa maharamia na walevi wa madaraka.
Wenu katika uwakilishi wa wananchi.
John Mnyika (Mb)
02/10/2014
02/10/2014
Chanzo: Jamii Forums.
إرسال تعليق