Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee.
Mbunge
wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima
Mdee na wenzake tisa wamepelekwa katika Gereza la Segerea jijini Dar
baada ya kushindwa kutimiza baadhi ya masharti ya dhamana yao.
Mdee
na wenzake nane mapema leo walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, Dar na kukana tuhuma zinazowakabili.
Mdee
na wenzake hao wanashitakiwa kwa makosa mawili kototii amri za maofisa
wa polisi na kufanya maandamano kinyume na sheria Jumamosi iliyopita ya
Oktoba 4, mwaka huu.
Watapandishwa tena kizimbani hapo kesho Octoba 08,2014,saa 4 asubuhi.
(Habari na Deogratius Mongela/GPL)
|
إرسال تعليق