ARSENAL imepata pigo kubwa kufuatia habari za kitabibu kuwa kiungo wake Mesut Ozil atakosa mechi zote zilizosalia mwaka huu.
Nyota
huyo wa kimataifa wa Ujerumani alifanya kipimo cha MRI kuchunguza
tatizo la goti lake na ndipo ipobainika kuwa atalazimika kuwa nje ya
dimba kwa miezi mitatu.
Hapo kabla, Ozil mwenye umri wa miaka 25 hakuweza kufanya mazoezi na kikosi cha Ujerumani baada ya kulalamika maumivu ya goti.
Mchezaji
huyo wa zamani wa Real Madrid hakuonyesha dalili yoyote ya maumivu
katika miezi ya hivi karibuni na akaweza kucheza mechi tisa na kufunga
bao moja.
Post a Comment