MAJANGA ARSENAL!! MESUT OZIL OUT MPAKA 2015


Mesut Ozil will be missing for the remainder of 2014 after the German FA confirmed he had a knee injury
ARSENAL imepata pigo kubwa kufuatia habari za kitabibu kuwa kiungo wake Mesut Ozil atakosa mechi zote zilizosalia mwaka huu.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani alifanya kipimo cha MRI kuchunguza tatizo la goti lake na ndipo ipobainika kuwa atalazimika kuwa nje ya dimba kwa miezi mitatu.
Hapo kabla, Ozil mwenye umri wa miaka 25 hakuweza kufanya mazoezi na kikosi cha Ujerumani baada ya kulalamika maumivu ya goti.
Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid hakuonyesha dalili yoyote ya maumivu katika miezi ya hivi karibuni na akaweza kucheza mechi tisa na kufunga bao moja.

Post a Comment

أحدث أقدم