Licha
ya kwamba Marekani imekuwa nchi ambayo imeweka rekodi ya kutibu watu
wenye maambukizi ya ugonjwa huku wachache wakiripotiwa kufariki, bado
imetangaza mkakati madhubuti ambao umewekwa ili kuhakikisha wanadhibiti
Ebola.
Marekani imetangaza rasmi utaratibu mpya
ambao unaowalazimu abiria wanaosafiri kwa ndege kuingia nchini humo
wakitokea Afrika Magharibi, kushuka katika moja ya viwanja maalum vitano
ambavyo vimetengwa.
Utaratibu ambao Marekani imeuweka
unawalazimu wasafiri wote kutoka nchi za Liberia, Guinea na Sierra Leone
kuingia nchini humo kwa kupitia moja viwanja vya O’Hare Chicago, JFK,
Newark, Washington Dulles au Atlanta.
Marekani imeweka utaratibu huo ambapo
viwanja hivyo vina wataalamu na mashine maalum za kufanyia uchunguzi wa
virusi vya ugonjwa huo.
Leo kamati ya dharura ya WHO imefanya
mkutano huku lengo kuu likiwa ni kutathmini juhudi zilizofikiwa za
kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.
Japo WHO imetangaza kutekeleza mpango wa
chanjo ya kinga ya Ebola kaatika ukanda wa Afrika Magharibi mayumaini
bado ni madogo mpaka sasa ambapo zaidi ya watu 4,700 wameripotiwa
kufariki kwa ugonjwa huo.
Post a Comment