Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius
Likwelile na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania wakiwaangalia kwa mshangao
wakurugenzi hao wawili walipokuwa wakiingia hawapo kwenye picha.
Ujumbe
kutoka Tanzania ukimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha
na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile alipokuwa
akiwasilisha mapendekezo yake kwa Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika na
Bw. Peter Larose Mkurugenzi Mtendaji mpya anayeachiwa kiti.
Bw.
Denny H. Kalyalya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake
wa kundi namba 1 la Afrika na Bw. Peter Larose ambaye ndiye anachukua
nafasi hiyo wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile alipokuwa akiwasilisha
mapendekezo yake kuhusu hali halisi ya misaada.
…………………………………………….
Katika mkutano muhimu uliofanyika
jioni hii hapa mjini Washington DC. Kati ya ujumbe kutoka Tanzania
ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali
Dr. Servacius Likwelile na Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni Mkurugenzi
Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika pamoja na Bw.
Peter Larose ambaye ndiye anachukua nafasi hiyo ulimpatia nafasi nzuri
sana Dr. Likwelile kuweza kueleza mambo muhimu ambayo Benki ya Dunia
ingepaswa kuyafahamu.
Katika mawasilisho yake katibu Mkuu huyo aliwaeleza viongozi wa
Benki ya Dunia kuwa ,anashukuru kwa ushirikiano mkubwa ambao ameupata
kutoka Benki ya Dunia na kusema kuwa hii imeisaidia sana Tanzania katika
kupiga hatua kiuchumi. Akiendelea kuzungumza Dr. Likwelile alisema kuwa
pamoja na kufanikiwa katika ushirikiano huo kumekuwa na tatizo ambalo
lina sababisha kuchelewa kwa utekelezaji wa Bajeti. Hili amelieleza kuwa
linatokana na masharti ya wafadhili kutaka kwanza mambo yanayohusu IPTL
kupatiwa ufumbuzi , kitu ambacho hakikuweko kwenye makubaliano. “ IPTL
haina uhusiano na makubaliano ya awali suala hili limeingia katikati hii
inaathiri utekelezaji wa kibajeti.”alisema. Aidha aliendela kueleza
kuwa sera ya Benki ya Dunia inadai kuwa kabila la Kimasai limetengwa na
hivyo kutaka baadhi ya miradi isiende sehemu nyingine zaidi ya umasaini,
hii nayo ni changamoto nyingine”. Katika mazungumzo hayo ilionekana
kweli kuwa kwa kuchelewesha kutoa fedha kwa ajili ya miradi kunachangia
sana kurudisha nyuma maendeleo.
Kwa mapendekezo haya mawili makubwa kama yatafikishwa kwenye
ngazi ya juu na yakafanyiwa kazi basi nchi yetu itapiga hatua kama
ilivyojipangia. Wakurugenzi hao waliyapokea mapendekezo hayo kwa mikono
miwili na wakaahidi kuyafikisha na kuyafanyia kazi.
Post a Comment