Katika
hali isiyo ya kawaida,watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wamevamia
Kanisa la PAG tawi la Kagemu kata ya Kitendaguro manispaa ya Bukoba na
kumua muumini mmoja kwa kumcharanga mapanga hadi kufa na mwenzake
kujeruhiwa, hawakuiba chochote ikiwemo simu zao.
Hata hivyo tukio hilo linahusishwa na imani za kidini kwamba waliohusika na tukio hilo ni wapinzani ya dini yao.
Mtoa
habari aliyegoma kutaja jina amesema chanzo cha mgogoro huo na kifo cha
muumini ambaye ni mwalimu katika shule ya sekondari KAGEMU ni baada ya
marehemu kuoa mwanamke wa dini nyingine (inaifadhiwa) na kumbadilisha
dini huyo mkewe na hapo waumini wa dini ya mkewe walianza vitimbwi kwa
kanisa hilo na hadi mauaji hayo kumekuwa na vurugu za kila mara baina ya
pande mbili.
Polisi
bado wanachunguza na watatoa taarifa baadae,mwili wa marehemu
umeifadhiwa katika chumba cha maiti bukoba mjini,majeruhi amelazwa
hospital ya mkoa.
Viongozi wa makanisa ya PAG walitarajiwa kutoa tamko rasmi mchana wa leo.
Post a Comment