Mwanaharakati Malala Yousafzai.
Mwanaharakati
mwenye umri mdogo kutoka nchini Pakistan, Malala Yousafzai pamoja na
mwanaharakati mwingine wa maswala ya watoto nchini India Kailash
Satyrathi, wameshinda tuzo ya amani ya Nobel.
Malala
mwenye umri wa miaka 16, ni mshindi mdogo zaidi kuwahi kushinda tuzo
hiyo katika historia yake.Malala amekuwa akiendeleza harakati zake za
kutaka watoto wa kike kuweza kupata elimu.
Alipigwa risasi kichwani na kundi la Taleban nchini Pakistan mwaka 2012 kwa kutetea wasichana kupata elimu.
Post a Comment