Marais
wa Liberia ,Sierra Leone na Guinea,mataifa matatu yalioathirika vibaya
na Ebola wanataka msaada zaidi ili kuwasaidia kukabiliana na ugonjwa wa
Ebola.
Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma ameiambia banki ya
dunia katika mkutano mjini Washington kwamba jamii ya kimataifa
haijachukua hatua za dharura kwa kuwa watoto wanaendelea kuwa
mayatima,huku madaktari na wauguzi wakifariki.
Naibu wa shirika la
afya duniani Bruce Aylward ameuambia mkutano huo kwamba Ebola imesambaa
katika miji yote mikuu ya mataifa hayo matatu yalioathirika pakubwa na
kwamba ulikuwa unaenea kwa kasi katika kila eneo.
Afisa mkuu wa
matibabu nchini Marekani Thomas Frieden amesema kuwa mlipuko wa Ebola
hauwezi kufananishwa na ugonjwa mwengine tangu kuzuka kwa ugonjwa wa
ukimwi.
إرسال تعليق