Meneja
wa mradi wa CIRDA kutoka UNDP, Bonizella Biagini akizungumza wakati
akitambulisha maofisa waliokuwepo katika uzinduzi wa warsha ya siku
tatu ya kimataifa ya ukusanyaji na matumizi ya taarifa ya hali ya hewa
kwa nchi 12 duniani. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa mataifa la Mipango ya maendeleo duniani (UNDP) Phillippe
Poinsot, Mwakilishi wa Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira
Binilith Mahenge, Bw. Richard Muyungi.
Na Mwandishi wetu
MATAIFA
11 ikiwemo Tanzania yanakutana jijini Dar kwa mafunzo ya siku tatu
yanayohusu utengenezaji wa mifumo bora ya upatikanaji wa taarifa za hali
ya hewa,uchakataji wake na matumizi ya taarifa hizo kwa wananchi wa
kawaida na watunga sera ili kuwa na uhakika na Mipango ya maendeleo.
Mataifa
hayo ni yale yalioyopo katika mradi wa Multi Country Support Programme
to Strengthen Climate Information Systems in Africa (CIRDA).
Nchi
zinazohusika katika mpango huu pamoja na wenyeji Tanzania ni Benin,
Burkina Faso, Ethiopia, the Gambia Liberia, Malawi, Sierra Leone, Sao
Tome and Principe,Uganda na Zambia.
Mpango
wa CIRDA unafadhiliwa na Global Environment Facility (GEF) na Least
Developed Country Fund (LDCF) ukilenga kuwezesha utumiaji wa teknolojia
mpya miongoni mwa wakulima, watunga sera na sekta binafsi ili kuweza
kufanya maamuzi sahihi kwa kuzingatia taarifa sahihi za hali ya hewa.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mkazi wa UNDP,Phillippe Poinsot Mpango wa CIRDA,
ambao ni mfano wa kuigwa kwa juhudi za mataifa ya Afrika ya kuwa na
ubadilishanaji wa maarifa na taarifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa,
huzingatia uhusishaji wa sekta binafsi, matumizi ya simu na takwimu za
kilimo (agricultural index insurance).
Akifungua mafunzo hayo, kwa niaba ya waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
rais, mazingira Binilith Mahenge, Ofisa anayeshughulikia mradi huo
nchini Richard Muyungi alisema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka
ambapo dunia nzima iko katika changamoto kubwa ya mabadiliko ya
tabianchi.
Alisema
Mafunzo hayo ambayo yanazinduliwa nchini yatajenga uwezo wa wataalamu
wa kubadilishana maarifa ili kuona kwamba wananchi wanafaidika na
utaalamu uliopo.
Alisema
Tanzania ikiwa inategemea zaidi wakulima katika uchumi wake ufikishaji
wa taarifa za hali ya hewa katika ngazi za chini na kwa usahihi ni
muhimu.
Alisema
program ya CIRDA ni mwenedelezo wa juhudi za serikali ya Tanzania
katika kushirikiana na mataifa mengine, kuimarisha mikakati ya
kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kw akuongeza uwezo na weledi
miongoni mwa wananchi wake na wadau wa hali ya hewa.
Kutokana
na hali hiyo Muyungi, alisema Tanzania inafuraha kufanyakazi na UNDP
kwa lengo la kuhakikisha kwamba taarifa za hali ya hewa na hadhari ya
awali ya uwapo wa majanga zinawafikia wananchi na zinatumika kwa ajili
ya maendeleo ya taifa.
Ndugu Abbas Kitogo Afisa Miradi ya Mabadiliko Tabia nchi kutoka UNDP akijitambulisha kwa washiriki wa warsha.
Kwa
mujibu wa Muyungi Tanzania inashirikiana na UNDP kuboresha upatikanaji
wa takwimu zinazotakiwa za hali ya hewa ili kupunguza madhara ya
mabadiliko ya hali ya hewani katika sekta za maendeleo.
Warsha
hiyo inayofanyika katika hoteli ya Whitesands imelenga kutoa na
kubadilishana utaalamu wa namna ya kuhudumia wananchi kupitia data
zinazotolewa na mamlaka za hali ya hewa na taasisi za kukabiliana na
majanga.
Akisisitiza
umuhimu wa mafunzo hayo Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Philippe Poinsot
ambaye alimwakilisha mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini,Alvaro Rodrigues alisema uzinduzi wa programu hiyo umelenga
kuimarisha upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa na hadhari za awali za
majanga kwa manufaa ya wananchi wa mataifa hayo.
Naye
meneja wa CIRDA, Bonizella Biagini, alisema watengeneza sera, wakulima
na wananchi wa Afrika wanahitaji takwimu za hali ya hewa za kisasa na
zinazotolewa kisayansi kwa kasi na kwa namna wanavyoweza kuzitafsiri
iliwaweze kufanya mipango yao ya muda mrefu ya maendeleo.
Mwakilishi
wa Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Binilith Mahenge,
Bw. Richard Muyungi akifungua mafunzo hayo ya siku tatu kwa wataalamu
wa hali ya hewa, mabadiliko ya tabia nchi na wanaojihuisha na majanga
kutoka nchi 12 ikiwemo Tanzania katika mpango wa CIRDA.
CIRDA
ni mpango wa kiutafiti wa mfumo wa hali ya hewa na mabadiliko yake
unaozingatia upatikanaji wa data za hali ya hewa na kuzifikisha maeneo
husika kwa matumizi kwa wakati.
Mradi
huo umelenga kuhakikisha wakulima, watunga sera na sekta binafsi
wanafanya maamuzi kwa kuzingatia taarifa za hali ya hewa kutokana na
mabadiliko makubwa yaliyopo sasa.
Mabadlikiko
ya tabia nchi yamefanya nchi nyingi kukumbwa na hali ya hewa mbaya kwa
maana ya kuvuruga uasili wa mazingira na kusababisha adha katika kilimo
na uvuvi.
Mafunzo
hayo yamelenga kuangalia teknolojia iliyopo sasa na namna ya kutumia
teknolojia hiyo kutoa tija katika kutengeneza na kutathmini taarifa za
hali ya hewa kwa lengo la kuimarisha mipango ya maendeleo ya taifa.
Mkurugenzi mkazi wa UNDP Philippe Poinsot akihutubia katika warsha hiyo.
Mapema
mwakilishi wa UNDP Tanzania alisema Tanzania ni mojawapo ya nchi
ambazo zinaathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa na mafunzo yatasaidia
kuepuka adha za mabadiliko ya hali ya hewa kwa wananchi vijijini hasa
kwa kuzingatia kwamba wananchi wake wengi wanategemea kilimo.
Alisema
kukosekana kwa taarifa za hali ya hewa kunafanya wananchi waliopo
vijijini kutokuwa na uhakika na maendeleo yao na kuwa katika hatari ya
kuyumbishwa na majanga mbalimbali.
Alishukuru
kwamba wataalamu wa kimataifa wanafanyakazi na serikali ya Tanzania kwa
lengo la kuhakikisha kwamba taarifa za hali ya hewa zinapatikana na
kutumiwa kusaidia mipango endelevu. (1) Ndugu Abas Kitogo Afisa
Miradi ya Mabadiliko Tabia Nchi kutoka UNDP Akijitambulisha kwa
washiriki wa warsha.
Washiriki wa warsha hiyo wakisikiliza mada kwa makini.
Ndugu Pascal F.Waniha mwakilishi wa mkurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa akitoa mada wakati warsha hiyo.
Meza kuu wakipiga makofi.
Mmoja
wa watoa mada Jeremy Usher kutoka CIRDA akiwasilisha mada kuhusu
umuhimu wa takwimu na uangaliaji wa mifumo katika dunia inayokabiliwa na
mabadiliko ya tabia nchi.
Sehemu ya washiriki kutoka nchi kumi na moja zinazoendelea kiuchumi wakifuatilia warsha.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ndugu Richard Muyungi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.
Post a Comment