Vitu vitatu vinavyoweza kukusaidia kupata kazi unayohitaji

Unataka kwenda kwenye ajira ambayo huijui au huna uzoefu nayo. Mara nyingi kutokuwa na uzoefu ni kitu ambacho kinawasumbua wengi na wakati mwingine unajihisi huwezi kupata fursa au kazi fulani.
SA-image-business-woman-2
Kama unataka kupata ajira mpya kwenye kampuni fulani, unatakiwa kujua utaleta kitu gani kwenye nafasi hiyo unayopewa. Si mara zote wanahitaji mtu mwenye uzoefu ila mtu amabaye yuko tayari kufanya kwa viwango vyao hata kama hana uzoefu ndio maana wanatoa miezi mitatu ya majaribio.
Hebu angalia sababu hizi zinaweza kukusaidia kupata kazi hata kama huna uzoefu;
  1. Unahitaji kuona Mambo kitofauti kutokea ngazi ya chini
Wote tunaanzia chini wakati fulani, hivyo kile unachokifanya sasa si lazima kuwa ndio hicho utakachokifanya maisha yako yote. Hivyo unatakiwa kubadilisha mfumo wako wa kufikiri unapoanza kutafuta kazi. Fanya kitu ambacho ni kidogo ambacho kitakuongezea uzoefu ule unaohitajika kwa kazi fulani. Hakuna kitu kidogo au ukasema huna uzoefu ila ni jinsi gani unafanya mambo yako kwaajili ya kukupa uzoefu.Unapoanza bila kitu katika kitu ambacho unakitaka katika taaluma au biashara ingawa wengi tunaogopa mabadiliko na kushindwa. Usiogope fursa kabla haujaijaribu, unahitaji kuanza mahali fulani ili uweze kuelekea sehemu nyingine. Ni kweli huna uzoefu je unafanya nini ili kukusaidia kupata uzoefu wa ile kazi unayoiota?
  1. Unatakiwa kuwa mbunifu katika fikra zako hicho ndicho kitu cha muhimu
Uwezo wako wa kuboresha ni kitu muhimu unapoboresha na kuendeleza taaluma yako. Haijalishi unataka kubadilisha taaluma au kupanda cheo unatakiwa kuwa mbunifu wa kila unachofanya ili uwe tofauti na mtu mwingine katika kitengo chako. Kwa lugha nyingine wewe unatofautishwaje na mtu mwingine mwenye cheti kama cha kwako?
Wahitimu wengi wa sasa hawajui teknolojia vizuri na wanaichukulia na kama kitu ambacho si cha muhimu sana mpaka uwe masomo ya sayansi. Kama unataka kuongeza ubunifu wako katika mawazo yako hakikisha unakwenda sambamba na teknolojia utajikuta fikra na mawazo yako yanakuwa tofauti na watu wengine katika eneo hilo hilo.
Ogopa kuwa mtu ambaye hujui nini kinaendelea kwenye teknolojia inayohusiana na kazi yako au taaluma yako unayoitaka. Unahitaji kujua program za komputa zinazohusiana na kazi yako vizuri, usisubiri kwamba utaenda kufundoshwa ukiajiriwa au kupata kazi ndipo unaanza kuhangaika kujifunza. Jifunze leo kiweze kukusaidia kesho.
  1. Kwasababu Wengine Wameweza na imewezekana
Mawazo yetu finyu wakati mwingine hufikiri mambo hayawezekani kwasababu hatujaona walioweza kufanikiwa au kufanya. Haimaanishi wewe kutojua kitu fulani basi watu wengine duniani hawajui kuhusu hicho bali unatakiwa ujue kama wewe hujui kuna mtu anajua na anaweza kukusaidia kutoka hapo ulipo kwenda hatua nyingine. Hutakiwi kukaa ukafikiri ni mwisho wa dunia hutotoka hapo, jaribu kufanya kitu na itawezekana hata kwa kujitolea fanya tu itakusaidia kukupa ujuzi. Kuna wengine wamepata kazi kwa sababu walijitolea kufanya kwa malipo ya kujikimu au kutolipwa kabisa na wakapata uzoefu ambao ukawasaidia kufikia ile kazi walioitamani. Kama huna uzoefu unafanya jitihada gani kutafuta huo uzoefu na kazi unaohitaji?
Jifunze vitu mbali mabali ingawa huna uzoefu vitakusaidia kufikia malengo na hatua fulani unayoitamani. Usikae tu kama pakacha bovu, fanya kitu ushindani ni mkubwa sana.

Post a Comment

Previous Post Next Post