Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Leonidas Gama amekanusha uvumi ulioenea kuwa yupo mgonjwa wa Ebola mkoani humo.
Akizungumza na mwandishi wa habari wa Redio Sauti ya Injili katika
kipindi cha Dira kilichosikika hewani baada ya saa mbili usiku wa
Alhamisi, Oktoba 23, 2014, aliyemwambia kuwa zipo taarifa kuwa yupo
mgonjwa amegundulika na dalili za ugonjwa wa Ebola huko Shirimatunda,
Mhe. Gama amesema, “Msiwashitue watu bila sababu, hakuna Ebola”
Mwandishi: “Sasa anaumwa nini huyo mgonjwa kama siyo Ebola?”
Mwandishi: “Sasa kwa nini apelekwe Shirimatunda kama hana Ebola?”
Gama: “sasa hiyo waulize Waganga, lakini mimi nina uhakika taarifa zao ni kwamba hakuna mtu ana Ebola”
Mwandishi: “...taarifa ni kwamba kile kituo wamekiandaa kwa ajili ya
kuhifadhi wagonjwa wa aina hiyo, na ndiyo maana wamemtoa moja kwa moja
kutoka Uwanja wa Ndege wakampeleka Shirimatunda.”
Gama: “Hapana, si kweli. Usiwe na wasiwasi. Si hata wewe ukitiwa
wasiwasi kuwa una kipindupindu, si kwamba ndiyo una kipindupindu? Unajua
suala la tahadhari siyo kwamba ndiyo ukweli. Ni tahadhari. Maana yake,
unaweza ukachukua tahadhari kama kuna mtu ana wasiwasi. Kama unatiliwa
wasiwasi kwamba huyu bwana anaumwa kipindupindu, lazima wamwangalie je,
ana kipindupindu kweli? …kumwangalia kipindupindu siyo lazima awe na
kipindupindu.”
Post a Comment