Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akana kuwepo mgonjwa wa Ebola

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Leonidas Gama amekanusha uvumi ulioenea kuwa yupo mgonjwa wa Ebola mkoani humo.

 

Akizungumza na mwandishi wa habari wa Redio Sauti ya Injili katika kipindi cha Dira kilichosikika hewani baada ya saa mbili usiku wa Alhamisi, Oktoba 23, 2014,  aliyemwambia kuwa zipo taarifa kuwa yupo mgonjwa amegundulika na dalili za ugonjwa wa Ebola huko Shirimatunda, Mhe. Gama amesema, “Msiwashitue watu bila sababu, hakuna Ebola” 

 

Mwandishi:Sasa anaumwa nini huyo mgonjwa kama siyo Ebola?”

 

Gama: “Ana magonjwa ya kawaida. Unajua mtu unaweza kuwa na Malaria ukazidiwa, basi jibu la haraka kwa sababu inawezekana ni mtu wa nje, watu wanasema Ebola… ni majibu mepesi.”


Mwandishi: “Sasa kwa nini apelekwe Shirimatunda kama hana Ebola?”

Gama: “sasa hiyo waulize Waganga, lakini mimi nina uhakika taarifa zao ni kwamba hakuna mtu ana Ebola”

Mwandishi: “...taarifa ni kwamba kile kituo wamekiandaa kwa ajili ya kuhifadhi wagonjwa wa aina hiyo, na ndiyo maana wamemtoa moja kwa moja kutoka Uwanja wa Ndege wakampeleka Shirimatunda.”

Gama: “Hapana, si kweli. Usiwe na wasiwasi. Si hata wewe ukitiwa wasiwasi kuwa una kipindupindu, si kwamba ndiyo una kipindupindu? Unajua suala la tahadhari siyo kwamba ndiyo ukweli. Ni tahadhari. Maana yake, unaweza ukachukua tahadhari kama kuna mtu ana wasiwasi. Kama unatiliwa wasiwasi kwamba huyu bwana anaumwa kipindupindu, lazima wamwangalie je, ana kipindupindu kweli? …kumwangalia kipindupindu siyo lazima awe na kipindupindu.”

Post a Comment

أحدث أقدم