MSANII SHERRY MAGALI AFARIKI DUNIA!


 Msanii nyota wa filamu nchini Sherry  Charles Magali enzi za uhai wake.

Msanii nyota wa filamu nchini Sherry  Charles Magali akiwa hoi hospitalini Wodi Namba 8 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro katika picha hii iliyopigwa na mwandishi wetu Ijumaa iliyopita, Okt 17, 2014.

Msanii huyo, amefariki leo saa nne asubuhi baada ya kuugua kwa muda mrefu. Kwa mujibu wa familia, taarifa zaidi za mazishi zitatolewa baadae. Global Publishers imekuwa ikifuatilia hali ya msanii huyu na kuwajulisha mashabiki wake mara kwa mara. Mara ya mwisho kuandika habari zake ilikuwa Februari 21 mwaka huu wakati alipokuwa amelazwa kwenye hospitali Kilimani maeneo ya Big Brother jijini Dar chini ya kichwa cha habari MTOTO WA MAGALI HOI KITANDANI.
Global Publishers inatoa pole kwa wafiwa na kumtakia marehemu alale pema- ameen!
PICHA NA STORI: DUSTAN SHEKIDELE - MOROGORO

Post a Comment

Previous Post Next Post