MTANGAZAJI WA TV ATUKANA WAKATI AKISOMA TAARIFA YA HABARI LIVE, AACHA KAZI NA KUONDOKA MUDA HUO HUO

Mtangazaji wa kituo cha TV cha KTVA, cha Alaska nchini Marekani, ametukana na kuacha kazi kwenye TV wakati akitangaza habari. Mtangazaji huyo, alikua akiripoti habari ya club ya wavuta bangi inayoitwa “Alaska Cannabis Club” au “Club ya Bangi ya Alaska.”

Sasa huyu dada wakati akitangaza habari ya club hiyo ya bangi, amejifichua na kusema yeye ndio mmiliki wa club hiyo, na kututana na kusema “fuck it. I quit.”
  • Tafsiri: “[tusi] naacha kazi”
  •  
  • Club hiyo inasaidia watu wanaotafuta bangi kubadilishana na kusaidiana jinsi ya kupata bangi; sababu sheria za jimbo hilo:
    • Zinaruhusu kuvuta bangi kwa sababu za kiafya kama una cheti cha daktari (medical marijuana)
    • Lakini haziruhusu kuuza bangi.
    Na hapo ndio kwenye tatizo la kisheria ambalo club hii, taasisi, pamoja na watu wengine wanapigia kampeni ibadilishwe sababu ni sheria isiyokuwa na mantiki. Utaruhusu vipi matumizi ya kitu, lakini upige marufuku mauzo yake? (Makahaba si wanaweza kutumia point hii pia kudai kuhalalishwa mauzo ya ngono? Lakini haya ni mengine; turudi kwenye stori) Kabla ya kutukana kwenye live TV na kuacha kazi, mtangazaji huyu amedai kuwa ameamua kujifichua kuwa yeye ndiye mmiliki wa club hiyo ya bangi (wakati akitangaza habari ya club hiyo hiyo…LOL,) na kuacha kazi ili atumie muda wake kutetea haki na uhuru wa wavuta bangi na kuanzia sasa atatumia nguvu zake katika jitihada hizo.
    Mawazo yangu: Lakini huyu dada si ameziharibia kampeni hizo za kutaka bangi iruhusiwe?Maana wapinzani wake wasiotaka bangi iruhusiwe si wanaweza kutumia kitendo chake kusema: “si unaona? Bangi isiruhusiwe maana inaharibu watu akili. Mtangazaji asiyevuta bangi hawezi kufanya kitendo cha kudhalilisha kwenye TV kama hiki”
    ANGALIA VIDEO YA TUKIO HILO


    Post a Comment

    أحدث أقدم