MWANAMKE MMOJA AUAWA BAADA YA KUPIGWA MATEKE, NGUMI WILAYANI RUNGWE

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 15.10.2014.
  • MWANAMKE MMOJA AUAWA BAADA YA KUPIGWA MATEKE NA NGUMI WILAYANI RUNGWE.
  • WAHAMIAJI HARAMU 07 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA.
  • JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKAZI WA IGAWILO WAKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU.
  • JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILO WAKAZI WA ILEMI WAKIWA NA NOTI BANDIA 23 NA DOLA 01 YA KIMAREKANI.
  • JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKAZI WA ILOLO WILAYANI MBOZI WAKIWA NA POMBE YA MOSHI LITA 15.
 KATIKA TUKIO LA KWANZA:
 MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA RUTINA NG’EKELE (75) MKAZI WA KIJIJI CHA MABONDENI ALIFARIKI DUNIA AKIWA ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA WILAYA RUNGWE BAADA YA KUSHAMBULIWA KWA KUPIGWA NGUMI NA MATEKE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA MTU AITWAYE NICOLOUS AFYUSISYE.
 TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 14.10.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA MABONDENI, KATA YA BULYAGA, TARAFA YA TUKUYU MJINI, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA.
 AWALI, INADAIWA KUWA MNAMO TAREHE 04.10.2014 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI MTUHUMIWA ALIMJERUHI MAREHEMU KWA KUMPIGA NGUMI NA MATEKE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUPELEKEA KULAZWA HOSPITALINI HAPO KWA MATIBABU HADI ALIPOFARIKI DUNIA MNAMO TAREHE 14.10.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA.
 CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI BAADA YA MAREHEMU KUMLIPA MTUHUMIWA TSHS. 7,000/= BADALA YA TSHS. 10,000/= ALIZOKUWA AKIDAIWA, HALI ILIYOPELEKEA MTUHUMIWA KUANZA KUMPIGA NA KUMJERUHI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
 TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA, WAHAMIAJI HARAMU 07 RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI KINYUME CHA SHERIA.
 WAHAMIAJI HAO NI PAMOJA NA 1. ADMASU ESCHAMO (18), 2. CHEKEBO DOLAMO (20), 3. INUGSE ABOSE (19), 4. GIRMA ABIYO (20), 5. DASALIN MASHA (18) 6. ABAYIN ARFICHO (19) NA 7. WORKICHO KADIRI (18) WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA.
 WAHAMIAJI HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 14.10.2014 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO KATIKA VICHAKA VYA ENEO LA STAMICO, KATA YA BUSALE, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAGENI NA WAHAMIAJI KUFUATA TARATIBU ZILIZOWEKWA KISHERIA ZA KUINGIA/KUHAMIA NCHINI ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.
KATIKA MSAKO WA PILI, WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. LUKA SAINI (23) MKAZI WA UYOLE NA 2. FURAHA SWEETMOND (25) MKAZI WA IGAWILO WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI AINA YA BOSS KATONI 02.
 WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 13.10.2014 MAJIRA YA SAA 13:30 MCHANA HUKO MAENEO YA UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WAUZAJI WA POMBE HIZO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII/WAFANYABIASHARA KUACHA KUJIHUSISHA NA UINGIZAJI NA UUZAJI WA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
 KATIKA MSAKO WA TATU, WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. BARAKA MWASHILINDI (26) MKAZI WA ILEMI NA 2. GIFT MWAGOZI (25) MKAZI WA KAGERA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA NOTI BANDIA ZA TSHS. 10,000/= ZIPATAZO 23 ZENYE THAMANI YA TSHS.230,000/= NA DOLA 01 YA KIMAREKANI YENYE THAMANI YA DOLA 100.
 WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 13.10.2014 MAJIRA YA SAA 12:30 MCHANA HUKO MAENEO YA UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
 NOTI HIZO BANDIA ZILIKUWA NA NAMBA ZIFUATAZO, BV 7213584 NOTI 01, BV 7213583 NOTI 02, BV 7213586 NOTI 03, BV 7213587 NOTI 02, BV 7213597 NOTI 01, BV 7213574 NOTI 01, BV 7213568 NOTI 01, EB 3657678 NOTI 05, EB 3657675 NOTI 03, EB 36577676 NOTI 02, EB 3657679 NOTI 02 NA DOLA YA MAREKANI YENYE NAMBA HK 20620722F. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU AU MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI NA USAMBAZAJI WA NOTI BANDIA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
 KATIKA MSAKO WA NNE, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. MPOKI SEME (34) MKAZI WA ILOLO NA 2. RICHARD MWALINDU (28) MKAZI WA ILOLO WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 15.
 WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 13.10.2014 MAJIRA YA SAA 11:30 ASUBUHI HUKO MAENEO YA ILOLO, KATA NA TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WATENGENEZAJI, WAUZAJI NA WATUMIAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI NA NI KINYUME CHA SHERIA.
 Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Post a Comment

Previous Post Next Post