Kijana mwendesha pikipiki akibeba
abiria maarufu kama (Boda boda) katika manispaa ya Tabora ameuawa na
watu wasiojulikana na kumtelekeza aneo la kanisa katholiki Makokola, na
kutoweka na pikipiki yake aina ya Sanlg huku kisu kilichodaiwa kutumika
kumuua kikitelekezwa eneo hilo.
Akizungumza kwa masikitiko eneo la tukio alipouawa mwendesha
pikipiki huyo, katibu wa chama cha waendesha Bodaboda Bw.Kasim Kiduli
amesema kuwa, matuikio ya kukatisha maisha ya waendesha pikipiki
inaonesha kurudi mkoani Tabora, kwani kulikuwa na ukimya kwa muda.
Baadhi ya wananchi wakiokuwa katika tukio hilo pamoja na kukemea
tabia ya mauaji, wamewataka waendesha pikipiki hao kujihadhari na
kutofanya kazi nyakati za usiku, kwani katika kubeba unaweza kumbeba
adui bila kumjua.
Kamanda wa polisi mkoani Tabora kamishina msaidizi Suzani Kaganda,
amemtaja marehemu kwa jina la Cosmas John, amesema kuwa, pamoja na kifo
hicho, katika hali isiyokuwa ya kawaida watu wasiojulikana wamewaua
mama na watoto wake wawili wanafunzi wa shule ya msingi Mwamalulu
wilayani Nzega.
إرسال تعليق