MWILI WA DK. WILLIUM SHIJA WAWASILI NCHINI HII LEO

 Mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Bunge la Jumuiya ya Madola (CPA), Dk William Ferdinand Shija umewasili nchini leo ikiwa ni siku saba tangu afikwe na umauti Oktoba 4, 2014. Shija aliyezaliwa Aprili 28, 1947 na kufariki Oktoba 4, 2014.
Imeandikwa na Father Kidevu.


Shija amewahi kuwa mbunge wa CCM wa jimbo la Sengerema toka mwaka 1990 hadi 2005. Alichaguliwa katika kikao cha 52 cha bunge hilo linalowakutanisha wawakilishi 700 kutoka mabunge ya nchi zilizo wanachama wa Jumuiya ya Madola.
Miongoni mwa viongozi waliofika kumpokea ni Pamoja na Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashilila, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Mchemba, Mama Kate Kamba, maofisa wa mbalimvbali wa Bunge na ndugu jamaa na maafiki.
Sanduku lililohifadhi mwili wa Marehemu Dk. Willium Shija.
 Maaskari wa Bunge wakifunika Sanduku lililohifadhi mwili wa marehemu.
 Getrude Shija akifarijiwa na ndugu jamaa na marafiki uwanjani hapo.
 Mjane wa aliyekuwa,Katibu Mkuu wa Bunge la Jumuiya ya Madola (CPA), Dk William Shija, Getrude Shija (katikati) akisaidiwa na marafiki zake, Elizabeth Cheyo (kushoto) na Anna Abbdalah baada ya kuwasili na mwili wa muwe jana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam.
Gari lililosafirisha mwili wa marehemu kutoka Uwanjani hadi nyumbani kwake.

Post a Comment

أحدث أقدم