Dar es Salaam. Ndanda iliyopanda daraja msimu
huu inarejea kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona
kuikabili Ruvu Shooting, huku kocha mkuu wa timu hiyo, Dennis Kitambi
akiwataka mashabiki kuujaza uwanja ili wapate ushindi wa kishindo.
Mechi zote tatu za Ligi Kuu Bara ilizocheza timu
hiyo dhidi ya Stand United, Mtibwa Sugar na Coastal Union, imecheza nje
ya mkoa wao na sasa itarejea Jumamosi ikipewa nguvu kubwa na mashabiki
wao ambao wamepanga kuifunika kabisa Mbeya City kwa ushangiliaji.
Kocha wa timu hiyo, Kitambi aliliambia gazeti hili
jana kuwa anaendelea kujifua na kurekebisha baadhi ya makosa
yaliyosababisha kufungwa mechi mbili zilizopita.
Kitambi alisema anatambua watakuwa nyumbani hivyo
atapata nguvu kubwa kutoka kwa mashabiki na kuwataka kufika kwa wingi
uwanjani kuwapa moyo ili waweze kushinda mchezo huo.
“Tunaendelea na maandalizi yetu vizuri, tumepoteza
mechi mbili mfululizo, hilo si jambo zuri lakini hakuna haja ya kukata
tamaa kwani ligi bado mbichi tunayo nafasi ya kujipanga ukizingatia sisi
ni wageni kwenye ligi.
“Tunachofurahi ni kwamba mechi ijayo tutakuwa nyumbani, tutapata nguvu,” alisema Kitambi.
Post a Comment