Lori aina ya Scania namba T 607 CWV Semi Taller (kama linavyoonekana
katika picha) lililokuwa limebeba kokoto limeanguka katikati ya lami
muda huu katika eneo la Chalinze Mzee Mkoani Pwani na kuharibika vibaya.
Kwa
mujibu wa Mashuhuda, ajali hiyo ametokea baada ya gari hilo lililokuwa
likielekea Dar es Salaam, kuteleza kutokana na mvua iliyonyesha asubuhi
ya leo mkoani humo.
Hata hivyo askari wa usalama barabarani wamefika eneo la tukio na
kufanikiwa kuliondoa gari hilo ambalo limesababisha foleni kubwa ya
magari yaliyokuwa yakitokea jijini Dar es Salaam kwenda mikoa ya Tanga,
Kilimanjaro na Arusha kutokana na kuziba barabara.
Post a Comment