Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Taasisi
na mashirika ya kimataifa yanayojihusisha na masuala ya mafuta na gesi
yameanza kujitokeza kuomba fursa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
ya kutaka kuwekeza katika sekta ya mafuta na Gesi.
Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Al
Iddi akikagua mradi wa maji safi na salama wa Kijiji cha Kichungwani
Jimbo la Kitope mara baada ya kushiriki kazi za ujenzi wa Taifa za
kulaza Bomba la Maji.
Alisema maombi ya mashirika na Taasisi hizo yamekuja kufuatia suala la mafuta na gesi kutolewa katika mambo ya Muungano kwenye katiba iliyopendekezwa na bunge maalum la Katiba lililomaliza kazi zakehivi karibuni Mkoani Dodoma.
Alisema maombi ya mashirika na Taasisi hizo yamekuja kufuatia suala la mafuta na gesi kutolewa katika mambo ya Muungano kwenye katiba iliyopendekezwa na bunge maalum la Katiba lililomaliza kazi zakehivi karibuni Mkoani Dodoma.
Balozi Seif ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kitope alitoa kauli hiyo
mara baada ya kushiriki katika kazi za ujenzi wa Taifa za kulaza Bomba
la Maji safi katika Kijiji cha Kichungwani lililoanzia katika Kijiji cha
Kitope.
Kazi hiyo ilikwenda sambamba na Balozi Seif kukabidhi Vipando vya
usafiri aina ya Vespa kwa ajili ya kuwarahisishia kazi Viongozi wa wadi
Nne zilizomo katika Jimbo la Kitope pamoja na kukabidhi msaada kwa
familia Tatu zilizokumbwa na maafa ya upepo pamoja na moto ukapelekea
nyumba zao kuathirika.
Vifaa pamoja na mchango huo wa Balozi Seif uliojumuisha pia fedha za
ununuzi wa madirisha ya Tawi la CCM Kichungwani na Timu ya Soka ya
Kijiji hicho umegharimu jumla ya shilingi za Kitanzania Milioni
16,850,000/-.
Balozi Seif alisema wananchi hao pamoja na Wazanzibari wote wana fursa
za kuunga mkono juhudi zilizochukuliwa na Wabunge wa Bunge Maalum la
Katiba za kuiunga mkono Katiba iliyopendekezwa kwa kuipigia kura ya ndio
itapowasilishwa kwao wakati wa kura ya maoni.
“ Nawaomba Wananchi na wapenda amani wote nchini kuiridhia Katiba
iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba ili imalize kiu iliyokuwepo
kwa muda mrefu “. Alisema Balozi Seif.
Alifahamisha kwamba Katiba hiyo itatoa nafasi na fursa pana kwa Zanzibar
katika kuimarisha mfumo wake wa kiuchumi na ustawi wa jamii mambo
ambayo yatawezesha kuondoa kabisa kero za muungano.
Alieleza kwamba Zanzibar endapo katiba hiyo itakubalika kwa umma itaweza
kufanya mashirikiano ya moja kwa moja na Taasisi, jumuiya na hata
mataifa mbali katika kujiletea maendeleo yake.
Alisema mfumo huo utampa haki Waziri au Kiongozi ye yote wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kwenda popote Duniani kutafuta mkopo au misaada
bila ya kuingiliwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Balozi Seif liwapongeza Wananchi wa Kijiji cha Kichungwani kwa jithada
zao za kujiletea maendeleo yao pamoja na kuondosha kero zinazowakabili
likiwemo suala la maji safi na salama.
Aliwahakikishia wananchi hao kwamba uongozi wa Jimbo hilo utakuwa tayari
wakati wote kuunga mkono jitihada za wananchi hao pamoja na kujaribu
kusaidia kuwatafutia wahisani wa kusaidia miradi yao.
Alisema juhudi za awali zimeshaanza kuchukuliwa na uongozi wa jimbo hilo
katika kutatua kero ya bara bara na huduma za umeme kwa kuziomba
taasisi zinazohusika na miradi hiyo kuchukuwa jitihada za kutatua kero
hizo huku akiwataka wananchi wenyewe wajikubalishe kuchangia miradi
hiyo.
Akigusia suala la ardhi ambalo limeingizwa ndani ya Katiba
iliyopendekezwa kuwa la Muungano Balozi Seif alisema hatua hiyo
imezingatia kutoa fursa kwa Wazanzibari kuweza kumiliki ardhi upande wa
Tanzania Bara ili waendelee kuimarisha harakati zao za kiuchumi.
“ Wazanzibari wapata hasara kubwa kama katiba iliyopendekezwa
hawataiunga mkono na kuipigia kura wakati utakapowadia “. Alisema Balozi
Seif ambae alikuwa Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Jimbo la
Kitope.
Naye Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi aliwaomba
wananchi hao kujikubalisha kuwa walinzi wa miradi yao ili kuwadhibiti
watu wanaojaribu kuvuruga miradi yao ya kiuchumi na ustawi wa jamii.
Mama Asha alisema wapo baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa wanaojaribu
kuwadanganya wananchi wasishiriki katika miradi yao ya maendeleo
wakijisahau kwamba wanasiasa hao sio viongozi bali ni watumishi wa
wananchi.
Mama Asha aliwaahidi Wananchi hao wa Kijiji cha Kichungwani kwamba
atakamilisha kuchangia maroli matano ya Mipira ya maji ili kukamilisha
mradi wao wa huduma za maji safi unaotokea katika Kijiji cha Kitope
hadi Kijijini pao Kichungwani.
Mapema Sheha wa Sheria ya Kitope Kichungwani Bwana Bakari Khamis Simai
alisema kwamba mradi huo wa maji safi na salama hivi sasa tayari umeanza
kuwafaidisha wananchi hao kwa zaidi ya robo tatu.
Bwana Bakari alieleza kwamba huduma za maji safi zilizokuwa kero na
usumbufu mkubwa wa muda mrefu kwa wakaazi hao wa Kichungwani hivi sasa
imekuwa ikipatikana katika pindi choche cha saa ishirini na nne.
Chanzo: zanzinews.com
Post a Comment