KATIKA hali isiyo ya kawaida, juzi mashabiki wa Simba walioonekana na machungu, walimvaa mshambuliaji Mganda wa timu hiyo, Emmanuel Okwi, huku wakimhoji kwa nini timu haifanyi vizuri.
Lakini shabiki mmoja, yeye alienda mbali, kwani alijitokeza mbele
akitaka kumfanyia fujo, jambo ambalo lilizua fujo na polisi kulazimika
kuingilia kati na kuwatawanya mashabiki hao.
Ilikuwa ni baada ya mechi dhidi ya Stand United kwenye Uwanja wa
Taifa, Simba wakiwa wametoka sare ya tatu mfululizo msimu huu.Juzi,
tafrani ilikuwa kubwa kwenye basi la Simba, mashabiki walilizingira na
kuanza kuwatolea maneno makali wachezaji, wakilalamika kwa nini
wanashindwa kufanya vizuri.
Lakini Okwi ndiye aliyeonekana kuzongwa zaidi na mashabiki hao waliokuwa wamepandwa na jazba.
Kama siyo polisi waliokuwa karibu na eneo hilo kuingilia kati, pengine hali ingekuwa mbaya zaidi.
Kama siyo polisi waliokuwa karibu na eneo hilo kuingilia kati, pengine hali ingekuwa mbaya zaidi.
Okwi bado hajafanya kile kilichotarajiwa na mashabiki wa Simba, baada
ya kutua msimu huu kwa usajili uliozua utata akitokea Yanga ambayo
ilikuwa na mgogoro naye.
Post a Comment