IKIWA ni
miaka 50 tokea kuanzishwa kwa skuli ya sekondari ya Fidel castro iliopo wilaya
ya Chakechake Pemba, bado skuli hiyo kongwe haina uzio, na kusababisha wananchi
kuingia katika maeneo hayo wakati wote, ambapo pichani ni kijana akiwa anawashikilia
watoto wawili ambao amedai wameingia eneo la skuli hiyo na kuiba suruwali moja
ya wanafunzi wakati ilipokua imefungwa kupisha sikukuu ya Eid el fitir (picha na Haji Nassor, Pemba)
HAKIMU wa mahakama ya mkoa Chakechake Khamis
Ali Simai, akifungua kongamano la maadhimisho ya siku ya kupinga adhabu ya kifo
duniani, kulia ni mwanasheria wa serikali Ali Hidari na kushoto ni kaimu
Mratibu wa ZLSC Khalifan Amour, ambapo limeandaliwa na kituo cha huduma za
sheria Zanzibar tawi la Pemba na kufanyika ukumbi wa chuo kikuu Zanzibar mjini
Chakechake Pemba (picha na Haji Nassor,
Pemba)
KAIMU Mratibu wa kituo cha huduma za
sheria Zanzibar ZSLC tawi la Pemba, Khalifan Amour akiahirisha kongamano la
siku ya kimataifa ya kupinga adhabu ya kifo, ambapo kongamano hilo lilifanyika
ukumbi wa chuo kikuu tawi la Pemba, kulia ni afisa mipango wa kituo hicho Safia
Saleh Sultan akifutiwa na mwanasheria wa serikali Ali Hidari (picha na Haji Nassor, Pemba)
BAADHI ya washiriki wa kongamano la kupinga
adhabu ya kifo duniani, lililoandaliwa na kituo cha huduma za sheria Zanzibar
tawi la Pemba, wakimsikiliza mtoa mada mwanasheria wa serikali Ali Haidar,
ambapo kongamano hilo lilifanyika mjini Chake chake (picha na Haji Nassor, Pemba)
Post a Comment