RAIS wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
amefanya Uteuzi wa Makadhi wa Wilaya za Unguja na Pemba.
Kwa
mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye
pia ni Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee Makadhi hao ni
Sheikh Ali Haruna Ramadhan-Unguja na Sheikh Abubakar Ali Mohamed-Unguja.
Wengine
ni Mohamed Ramadhan Khamis-Unguja na Sheikh Omar Juma Othman-Pemba. Rais
Shein amefanya Uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu
namba 5 cha Sheria ya Mhakama ya Kadhi Namba 3 ya mwaka 1985 kama
ilivyorekebishwa na Sheria namba 4 ya mwaka 2003.
Uteuzi huo umeanza Septemba 12,2014.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
Post a Comment