Wanawake wawili wameishitaki idara ya usalama ya Jimbo la Texas
kufuatia kusachiwa katika nyeti zao na askari waliowashuku kuwa
wameficha bangi.
Askari polisi David Farrell aliwasimamisha wanawake hao, Angel Dobbs,
38, na mpwa wake Ashley Dobbs, 24 kwa kudai wametupa uchafu barabarani
(vichungi vya sigara.)
Baada ya kudai amesikia harufu ya bangi, alimwita
askari wa kike, Kelley Helleson, kwa kutumia redio na kumuambia
awasachi wanawake hao makalioni na katika uke.
Ofisa Helleson anaonekana katika video akiingiza mkono wake katika
nyeti za wanawake hao wawili bila hata kubadilisha gloves kati yao.
Kesi hiyo imetatuliwa nje ya mahakama baada ya wanawake hao kukubali
kulipwa fidia ya $185,000 (takriban TShs milioni 306.za kitanzania)
Ofisa Farrell
alisimamishwa kazi, na Helleson alifukuzwa kazi kufuatia vitendo vyao
hivyo ambavyo ni kinyume na sheria.
إرسال تعليق