
TAARIFA tulizozipata
kutoka mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, zinasema jeshi la polisi nchini
limemkamata na kumfikisha katika mahakama ya kijeshi askari wake
Pc.Godlisen anayetuhumiwa kumtumikisha katika vitendo vya ngono
mwanafunzi wa kidato cha tatu wa shule ya sekondari Okaoni iliyopo
wilaya ya Moshi.

Habari zinasema
kuwa,askari huyo ambaye septemba 21 mwaka huu alimfungia kwenye nyumba
ya kulala wageni mjini moshi mwanafunzi huyo na baadaye wawili hao
kupata ajali mbaya ya pikipiki, aliumia kwenye moja ya bega lake na
hivyo kushindwa kupelekwa kwenye mahakama ya kijeshi.
Kaimu kamanda wa
liposi mkoa wa Kilimanjaro,Koka Moita, pamoja na kukiri kuwa wameanzisha
uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo, alikataa kuweka wazi kama askari
huyo amefunguliwa mashitaka ya kijeshi.
Kamanda Koka
amewaambia waandishi wa habari leo kuwa, jeshi la polisi linafanya
uchunguzi juu ya tuhuma hizo na kwamba kama itabainika,askari huyo
atachukuliwa hatua za kinidhamu kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa.
Pamoja na jeshi hilo
kumfungulia mashitaka ya kijeshi askari huyo,taarifa kutoka kwa mmoja wa
wazazi wa mwanafunzi hiyo zinadai kuwa,kuna juhudi za makusudi
zinafanywa na askari wa jeshi hilo kutaka kukwamisha mashitaka ya
kijeshi dhidi ya askari huyo.
Taarifa zinadai
kuwa,polisi wa kituo kikuu cha polisi mjini moshi,wanajenga ushawishi
kwa wazazi wa mwanafunzi huyo kutaka kulimaliza suala hilo kienyeji huku
hali ya mwanafunzi huyo ikielezwa kuwa mbaya kutokana na miguu yake
kuvimba.
Kwa taarifa zaidi endelea kutembelea mtandao huu wa
www.kalulunga.blogspot.com
Post a Comment