Polisi
nchini Brazili wamemkamata mwanamume mmoja aliyekiri kwa kinywa chake
kuua watu wapatao thelathini na tisa katika kipindi cha miaka mitatu.
Polisi
wamemuelezea mtu huyo kuwa ni mwenye umri wa miaka ishirini na sita
ambaye alikua mlinzi katika kampuni fulani alikuwa akiwawinda wa watoto
wa mitaani,wanawake na wapenzi wa jinsia moja.
Mwanamume Tiago
Gomes da Rocha alikamatiwa nyumbani kwake Goiania na polisi wa kikosi
maalumu waliokuwa wakichunguza mauaji hayo,na kuelezea namna walivyomtia
mkononi kuwa alihemewa na aliyoyafanya,
Kijana huyo alikuwa
akitekeleza mauaji yake kwa kutumia pikipiki huku akiwa ameuficha uso
wake kwa kutumia kofia ngumu ya pikipiki na kuwashambulia alowalenga, na
akikutana nao huwadai walichonacho kabla hajawapiga risasi na kuwaacha
wakijifia taratibu.
Post a Comment