Rais
wa Marekani Barack Obama amethibitisha wito wa kulitumia jeshi la nchi
hiyo na wale wa akiba iwapo watahitajika kupambana na mlipuko wa ugonjwa
wa Ebola Afrika magharibi.
Rais Obama amesema wanajeshi hao wataongeza nguvu ya jeshi katika kutoa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo.
Kundi
la kwanza la wanajeshi hao linatarajiwa kupelekwa kusaidia ujenzi wa
vituo 17 vya kutolea tiba ya ugonjwa huo, katikati mwa Liberia, moja ya
nchi iliyoathiriwa vibaya na ugonjwa huo.
Maafisa wa kikosi cha
ulinzi wameelezea agizo hilo la Raisi Obama kama agizo la muhumu ili
kuongeza kasi ya kutekeleza mipango ya kwenda kuisaidia mapambano ya
ugonjwa huo
na itamfanya rais kutuma majeshi mengine zaidi iwapo watahitajika.
Marekani
imeahidi kupeleka askari wake wapatao elfu nne huko Africa Magharibi
kusaidia mapambano ya kuzuia na kuumaliza kabisa ueneaji wa ugonjwa wa
Ebola.
Rais Obama amesema hajapinga wazo la kutekeleza katazo la
kuziuia watu wanaoingia nchini Marekani kutoka nchi zilizo athiriwa na
ugonjwa huo,na hadhani kama wazo hilo litafanikiwa.
Ameyasema hayo
mwishoni mwa mkutano aloufanya katika ikulu ya Marekani na maafisa wa
shirikisho juu ya ushiriki wa nchi ya Marekani katika mapambano na
ugonjwa huo.
Raisi Obama amesema anaamini hatua za uchunguzi wa ugonjwa huo ni hatua nzuri.
Sina
sababu za kifolosofia ya kupinga katazo la safari, kama hiyo ndiyo
itakuwa ndiyo njia bora ya kuwaweka raia wa Marekani salama.tatizo ni
kwamba je haya ndiyo majadiliano yangu niliyoyafanya a na wataalamu
walioko kwenye maeneo ya tukio yaliyoathiriwa na ugonjwa huo ni kwamba
katazo la safari halina nguvu kama hatua tulizochukua hivi karibuni
kupambana na ugojwa huo.
Obama pia aesema yupo wazi kumteua atakayesimamia janga la Ebola
Mpaka
hatua hii kila mtu binafsi amefanya kazi nzuri yenye kutukuka ,kazi
ambayo ni ngumu kupambana na majimaji ya ugonjwa huu. Hii inatufanya
tuwe kama mtu mmoja ,kwa sehemu baada ya janga hili tunaweza kusonga
mbele kama kawaida.
Naye mkuu wa kitengo cha maendeleo ya
kimataifa wa Marekani ameahidi kuongeza dola milioni mia moja na
arobaini na mbili ili kusaidia mapambano ya ugonjwa wa Ebola huko
Guinea.
Bwana Rajiv Shah aliyeko nchini Guinea kwenye ziara ya
kujionea hali halisi ya athari zilizoletwa na ugonjwa huo Africa
Magharibi, na kusema kwamba anafikiri msaada huo utarejesha matumaini ya
watu waishio nchini humo.
Natangaza ongezeko la dola milioni moja
na eflfu arobaini na mbili ili kuendeleza mapambano nchini Guinea
katika ugonjwa wa Ebola,kwa vitengo vinavyojihusisha na ugonjwa huu,ili
kuongeza ufanisi katika idara ya afya na wafanyakazi wake na kuongeza
nguvu katika elimu juu ya ugonjwa huu.
-BBC
Post a Comment