Na
Anita Jonas-MAELEZO
Umoja
wa Mataifa umeshauri kuchukua hatua za haraka kwa magongwa ya mlipuko yanayotokea
Afrika kama Ebola kwani yanadhiri uchumi wa mataifa husika.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka
wakati wa Maadhimisho ya Miaka 69 ya Umoja wa Kimataifa leo Jijini Dar es
Salaam.
Prof.
Tibaijuka alisema kuwa Umoja wa Mataifa wanatakiwa kuchukua tahadhari ya
milipuko ya magonjwa hatarishi na kuyachukulia kama ni magonjwa ya Kidunia
kwani yanaathiri mifumo yote ya kimaendeleo.
“Mataifa
yaliyoendelea yasingepuuzia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ulipojitokeza Afrika
hali isingekuwa hatarishi kama ilivyo sasa, hivyo ni rai
yangu kwa Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na mataifa husika kuchukua tahadhari wakati wote ”Alisema Prof.
Tibaijuka.
Aidha,
Prof. Tibaijuka alisema kuwa kutokana na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi
kuwa tishio miongoni mwa wengi duniani, wahisani wa maendeleo hawanabudi kusaidia
Mataifa mengine ikiwamo utekelezaji wa Mfuko wa Kijani wa Hali ya hewa.
Akizungumzia
kuhusu hatua ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete kutoa uraia kwa wakimbizi 162,000
kutoka Burundi, Prof. Tibaijuka alisema kuwa Tanzania imeonyesha ulimwengu kuwa
suala la mapambano dhidi ya ukimbizi linaweza kufanyiwa kazi na kuwafanya
wakimbizi kuishi maisha kama binadamu wengine.
Naye
Mratibu muwakilishi wa makazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
Bw. Alvaro Rodriguez alisema kuwa shirika hilo kwa kushirikiana na serikali na
wadau wengine, wamepanga kusaidia na
kuboresha miundombinu ya kiusalama ili kuendeleza amani Duniani kwani bila
amani maendeleo ni vigumu kupatikana.
Pia
Bw. Rodriguez aliipongeza Tanzania katika kutekeleza Malengo ya Millenia katika
sekta ya afya kwa ambapo asilimia 96 ya vituo vyote vya afya nchini vinatoa
huduma ya afya ya uzazi kwa mama na mtoto.
إرسال تعليق