Rais Jakaya Kikwete
akimpa cheti cha uraia wa Tanzania, Loveness Ruhaga (kulia) aliyekuwa Mkimbizi
kutoka nchini Burundi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi
ya Mkuu wa Tabora leo. Rais Kikwete alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 162,156
na kuwatangazia kuwa sasa wamekuwa raia halali wa Tanzania hivyo wahakikishe wanafuata
sheria zote za nchi na waepuke kufanya vurugu za aina yoyote kwani wakikiuka
masharti hayo waweza kunyanganywa uraia huo. Wakimbizi hao walioingia nchini
tangu mwaka 1972 walionyesha furaha kwa kuimba na kucheza vyimbo mbalimbali. Kushoto
ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.
Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (kushoto)
akimuonesha Rais Jakaya Kikwete (kulia) mchoro unaoonesha jinsi wakimbizi wa
Burundi walivyoingia nchini wakati walipokuwa wanatoka nchini kwao mwaka 1972. Rais
Kikwete alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 162,156 waliokuwa raia wa Burundi
katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa wa Tabora leo. Katikati
ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza
baada ya kuwapa vyeti vya uraia wa Tanzania, waliokuwa wakimbizi 162,156 kutoka
nchini Burundi walioingia nchini tangu mwaka 1972. Tukio la utoaji wa vyeti
hivyo lilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora
mjini humo leo. Raia Kikwete katika hotuba yake aliwataka raia hao wapya kuwa
waadilifu na kufuata sheria zote za nchi. Wanne kushoto ni Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Mbarak Abdulwakil na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison
Mseke.
Msoma risala ambaye
ni mwakilishi wa raia wapya 162,156 nchini ambao walikuwa wakimbizi kutoka
nchini Burundi, Dafroza Baragwimba akiisoma risala yao mbele ya Rais Jakaya
Kikwete (watatu kulia) wakati ya hafla ya utoaji wa vyeti kwa raia hao. Rais
Kikwete alitoa uraia kwa wakimbizi hao na kuwataka wawe waadilifu na kufuata
sheria zote za nchi. Wanne kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias
Chikawe.
Rais Jakaya Kikwete (wasita kushoto waliokaa),
mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa nchini, Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watano kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya
Wakimbizi, Harrison Mseke (watatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma
Mwassa (wasita kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya raia wapya 162,156
wa Tanzania (nyuma waliosimama) baada ya kupewa vyeti vya uraia na Rais Kikwete
katika hafla iliyofanyika katika ofisi
ya Mkuu wa Mkoa mjini humo. Picha zote na Felix Mwagara, wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Post a Comment