
Katibu
wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi Claudia Mpangala akiwaeleza waandishi wa
habari kuhusu Kongamano la maadhimisho ya Miaka 10 ya Tume hiyo tangu
kuanzishwa kwake ambapo Kongamano hilo litawahusisha Mawaziri,
KatibuMkuu Kiongozi na Watendaji Wakuu kutoka katika Wizara, Idara
zinazojitegemea,Taasisi na Mashirika ya Umma. Kulia ni Naibu katibu wa
Tume hiyo Bi NeemaTawale.

Katibu
wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi Claudia Mpangala akiwaeleza waandishi wa
habari kuhusu Kongamano la maadhimisho ya Miaka 10 ya Tume hiyo tangu
kuanzishwa kwake ambalo litafanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius K.
Nyerere tarehe 30 Oktoba, 2014 ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mhe.
Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kushoto ni Naibu Katibu wa Tume hiyo Bi Rose Elipenda na kulia ni Naibu
Katibu Bi Neema Tawale akifuatiwa na Naibu Katibu Bi Rose Mboya.
(Picha na Frank Mvungi-MAELEZO).
Frank Mvungi-Maelezo
Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi kongamano la maadhimisho ya Miaka 10 ya
Tume ya Utumishi wa Umma yatakayofanyika jijini Dar es salam Oktoba 30
mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Julius K. Nyerere.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Katibu wa Tume ya Utumishi wa
Umma Bi Claudia Mpangala wakati wa Mkutano na waandishi wa habari ulio
lenga kutoa ufafanuzi kuhusu maadhimisho hayo.
Akifafanua
kuhusu siku hiyo Mpangala amesema Kongamano hilo la siku moja litaanza
saa 2:00 asubuhi hadi 11:00 jioni ambapo pamoja na mambo mengine
kongamano hilo litahusisha historia ya Utumishi wa Umma kabla na baada
ya Uhuru.
“Kauli
mbiu katika maadhimisho hayo ni Imarisha Uzalendo,Uadilifu na
Uwajibikaji katika Kusimamia Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma ili
kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini” alisemaMpangala.
Akizungumzia
wageni watakaoshiriki Mpangala amesema kongamano hilo litawahusisha
Mawaziri, Katibu Mkuu Kiongozi, Watendaji Wakuu kutoka katika Wizara,
Sekretarieti za Mikoa, Idara zinazojitegemea, Taasisi na Mashirika ya
Umma, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wakuu wa Idara ya Utawala na
Rasilimali Watu.
Pia
Mpangala alitoa wito kwa waalikwa wote kuhudhuria kongamano hilo kwa
lengo la kuonaTume ilipotoka, ilipo na inapoelekea kwa kuyatazama
mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 10 na mwelekeo wa Tume
katika kipindi cha miaka 10 ijayo.
Tume
ya Utumishi wa Umma ilianzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 9 (1) cha
sharia ya Utumishi wa Umma NA. 8 ya mwaka 2002 ambapo kwa mujibu wa
kifungu cha 9 (3) cha sheria ya Utumishi wa Umma Na 8 ya mwaka 2002 kama
ilivyorekebishwa kwa sharia Na 18 ya mwaka 2007.
إرسال تعليق