Rais wa Nigeria atishia kuishtaki website iliyomtaja kwenye orodha ya marais tajiri Africa

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan ametishia kuishtaki website iliyomtaja kama mmoja wa marais 10 wa Africa matajiri zaidi.
Mtandao huo uitwao. richestlifestyle.com umemtaja Jonathan kama rais wa sita kwa utajiri wake wa dola milioni 100
Maelezo kutoka ofisi yake yamedai kuingizwa kwake kwenye orodha hiyo hakuna ukweli na ni jaribio la kutaka kumuonesha kama fisadi
Tayari website hiyo imemuondoa kiongozi huyo wa Nigeria kwenye orodha.
Rais Jonathan amekuwa akikosolewa kwa kutotangaza mali zake hadharani.
Ikulu ya nchi hiyo ilitishia kuchukua hatua za kisheria hadi pale website hiyo itakapoitoa makala hiyo au kuomba radhi.

Post a Comment

أحدث أقدم