Mkuu
wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akizungumza kwenye ufunguaji wa
warsha ya wadau kujadili rasimu ya mwisho ya taarifa ya mpango wa
usimamizi na uendelezaji wa pamoja wa rasilimali za maji wa bodi ya maji
ya bonde la kati, liyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aquar Vitae
hotel mjini Singida.
Na Abby Nkungu, Singida
MKUU
wa mkoa wa Singida, Dk Parseko Kone alilazimika kumtaka mshereheshaji
katika Warsha ya Wadau wa Rasimu ya Mpango wa Usimamizi na Uendelezaji
wa pamoja wa Raslimali za Maji Bonde la Kati kuacha kuendesha
utambulisho wa wajumbe hao kwa lugha ya kiingereza badala yake atumie
Kiswahili.
Dk
Kone alilazimika kuingilia kati baada ya kushuhudia baadhi ya wajumbe
waliokuwa wakitambulishwa na kutakiwa kusimama ili waonekane kushindwa
kufanya hivyo kwa kile kilichodhihirika wazi kupigwa na bubumbuwazi na
utambulisho huo wa lugha ya kiingereza.
Akionesha
wazi kukerwa kwake na mshehereshaji huyo, Dk Kone alisema kuwa wakati
taifa liko katika juhudi za kukuza Kiswahili nchini, baadhi ya
Watanzania wanakwamisha juhudi hizo kwa sababu hafifu kama za kuwepo
baadhi ya washiriki wasiojua kiswahili.
“Wajumbe
wa Warsha hii wako 200 na wasioelewa Kiswahili ni wanne tu. Idadi hii
ndogo haiwezi kusababisha mkutano huu uendeshwe kwa kiingereza. Wengi
wetu hapa japo tunajua kiingereza, baadhi yetu mwaka umepita bila
kukizungumza; hivyo inahitaji mtu kujiandaa ili kuwa katika nafasi
nzuri ya kukizungumza” alisema.
Aidha,
alisema kuwa endapo Warsha hiyo ingeendeshwa kwa lugha ya kiingereza,
wachangiaji wa Rasimu hiyo wangekuwa wachache hivyo kuwanyima wengi
fursa ya kutoa mawazo yao.
Baadhi
ya wadau waliohudhuria warsha ya wadau kujadili rasimu ya mwisho ya
taarifa ya mpango wa usimamizi na uendelezaji wa pamoja wa rasilimali za
maji wa bodi ya maji ya bonde la kati,iliyofanyika mjini Singida(Picha
na Nathaniel Limu).
Katika
hotuba yake ya ufunguzi Dk Kone aliwataka wadau wote kushirikiana
katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazokabili usimamizi wa
raslimali za maji kutokana na suala hilo kuwa mtambuka. Alizitaja baadhi
ya changamoto hizo kuwa ni migogoro inayohusiana na maji pamoja na
siasa.
Alisema
kuwa sekta ya maji ina jukumu kubwa katika maendeleo ya kijamii na
kiuchumi lakini kwa bahati mbaya inakabiliwa na changamoto mbalimbali
ambazo bila kutatuliwa huathiri utekelezaji wa mipango na mikakati ya
maendeleo na usimamizi wa raslimali za maji.
Bonde
la Kati lenye makao yake makuu mkoani Singida ni miongoni mwa mabonde
tisa yaliyopo nchini na linajumuisha maeneo ya Dodoma, Manyara, Singida,
Tabora, Shinyanga, Arusha na Kilimanjaro ambapo linagusa jumla ya
wilaya 26. Ni la pili kwa ukubwa likiwa na kilomita za mraba 143,099.
Post a Comment