Samsung Galaxy Note 4- simu iliyosubiriwa na watu wengi yazinduliwa Africa


samsung galaxy note 4 black
Macho yaelekea kwenye uzinduzi nchini Tanzania!
Kampuni ya Samsung imezindua toleo jipya la simu zake za Galaxy Note 4 Jijini Berlin Nchini Ujerumani Septemba 2014.  Toleo hilo la teknolojia ya kisasa katika orodha za simu aina ya Note inazidi kuimarisha kampuni ya Samsung na kuzidi kufanya vizuri katika soko la simu duniani. Siku ya tarehe 17 Octoba, 2014 Kampuni ya Samsung ilifanya uzinduzi  Mjini wa Cape Town- Afrika Kusini katika ziara ya Galaxy Note 4 Barani Africa.
Watanzania wanatarajiwa kupanga mistari katika maduka ya Samsung kushudia toleo jipya la simu katika familia ya Galaxy Note. Hii inatokana na uzinduzi mkubwa  uliyofanyika Cape Town-Afrika Kusini ambayo ilikua ni ishara ya upatikanaji wa simu  hizi za kisasa katika soko la Bara la Afrika na Tanzania ikiwemo.
Kutokana na  Uzinduzi mkubwa uliofanyika Berlin, simu hii imepata umaarufu mkubwa na kujulikana kama ‘‘muongozi wa mabadiliko katika ulimwengu wa simu (smartphones) za mkononi’’. Galaxy Note 4 mpya ina kioo kikubwa chenye ubora zaidi wa kuonyesha matukio, na kalamu (S Pen) ya kipekee inayompa mtumiaji  uhuru na uwezo mkubwa wa kutumia simu hiyo.
Uzinduzi Barani Afrika Ulihusisha viongozi mbalimbali wa kampuni ya Samsung duniani akiwemo Mh. Mike Seo Mkurugenzi Mtendaji wa Samsung Electronics Tanzania, pamoja na  mawakala wa Samsung, waandishi wa Habari na washiriki wengine.
samsung galaxy note 4.
Akiongea kwa hamasa kubwa kuhusu uzinduzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni katika soko la Tanzania Mh. Mike Seo alisema ‘‘ Tunatazamia kuleta toleo jipya la Galaxy Note kwa wateja wetu nchini  Tanzania. Kutokana na muunganiko wa Teknologia mpya na  maoni kutoka kwa wateja  wetu sasa tunaleta utamaduni wa kalamu na karatasi katika ulimwengu mpya wa teknologia ya kisasa nchini Tanzania’’
Uingiaji wa haraka wa  simu hii maeneo ya Kusini mwa Jangwa la Sahara ni ishara kubwa inayoonyesha  umuhimu mkubwa wa Africa  katika soko la dunia, kutokana  na watumiaji kutambua ukuaji wa teknolojia katika maisha yao. Hivi karibuni ukuaji na uwezo wa watanzania kwenye soko kunadhihirisha kuwa hawana haja ya kuendelea kusubiri simu hii kutiririka nchini miezi kadhaa baada ya kuzinduliwa kwenye mabara jirani kama Asia na Ulaya. Huitaji wa bidhaa zenye technolojia ya hali ya juu unazidi kuhongezeka na Samsung imejikita katika kuendeleza uhitaji huo wa Tekinolojia mpya inayopanda siku hadi siku katika nchi mbalimbali Barani afrika.
Ikifuatia mafanikio ya matoleo ya Galaxy Note, Duniani kwa ujumla Galaxy Note 4 inakidhi matarajio ya watumiaji. Kampuni ya Samsung ina matarajio makubwa ya simu hii ya kisasa katika soko la Tanzania na Afrika kwa ujumla. Simu hii inaakisi kile ambacho kampuni ya Samsung huona kama mchango muhimu unaotolewa na soko la Afrika katika soko la dunia.
samsung galaxy note 4
Samsung inawaahidi watumiaji wake ubora na utofauti wa kipekee kupitia Galaxy Note 4. Simu hii itapatikana kwa rangi mbali mbali kama Nyeusi, Nyeupe, Dhahabu, Pinki ikiambatanishwa na  kalamu ya simu ambayo huraishisha matumizi ya simu hiyo.
Wateja wote wanaweza kujua zaidi kuhusu simu hii kwa kupitia programu ya Galaxy Note 4 inayopatikana kwenye PlayStore au kutembelea maduka yoyote yaliyo idhinishwa na Samsung,
Baadhi ya sifa kuu ambazo watumiaji watafurahia kutumia Galaxy Note 4:
Kalamu (S Pen)
Imetengenezwa kisasa kumfanya mtumiaji kuandika kwa ubora. Uwezo mkubwa unamfanya mtumiaji kuhisi kama anaandika au kuchora  kwenye karatasi. Pia simu hii ina  uwezo wa kupiga picha maandishi na kuugeuza katika maandishi ndani ya simu.
Kamera
Simu  inakuja na camera ya nyuma yenye uwezo  wa MegaPixels 16 na Kamera ya mbele yenye uwezo wa Megpixels 3.7.Ina uwezo wa kujirekebisha yenyewe kulingana na hali ya hewa au eneo  kutoa picha Nzuri.
Betri
Simu hii ina uwezo wa kuchaji kuanzia asilimia 0  mpaka 50 kwa dakika 30. Kama ilivyo kwa simu aina ya Galaxy S5 simu hii pia  ina mfumo wa kutunza chaji  ambao unaruhusu kuhifadhi chaji kwaajili ya matumizi ya muhimu ya simu pale chaji inapoisha kabisa.
Hupunguza kelele
Inampatia mtumiaji uwezo wakuwasiliana kwa urahisi kutokana na uwezo wa simu kupunguza kelele za pembeni.
Ulinzi
Ina ulinzi wa alama za vidole ulioboreshwa zaidi  kwa ajili ya ulinzi wa taarifa binafsi za mmiliki wa simu.

Post a Comment

Previous Post Next Post