Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga Tanzania, na kusema mtu yeyote atakayepata kipingamizi aifahamishe Wizara yake kwa ufafanuzi zaidi:
“Tumejitosheleza kwa chakula kwa asilimia 125. Mahindi tumeongeza uzalishaji zaidi ya tani milioni 6, mchele tumezalisha tani milioni moja laki sita. Bado watu wanakuwa-confused maana kuna watu wanawaambia kwamba kuna kibali, kuna vizuizi vya kuuza nje. Sera hiyo tumeachana nayo. Sisi sera yetu ni ‘zalisha ziada, upate masoko, uza nje,’ kwa hiyo wanaotaka kuuza nje ya nchi ziada, alimradi wasiuze kila kitu mpaka chakula wasiweke akiba.”Mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga nchini Tanzania unatekelezwa kuanzia mwaka huu wa 2014 hadi mwaka 2017. Nchi nyingine za Afrika zinazotekeleza mkakati huo ni Nigeria, Ghana na Burkina Faso.
Post a Comment